UONGOZI wa timu ya Ashanti United ya Ilala ambayo ipo daraja la kwanza umesema unakifanyia marekebisho kikosi chao ili kuwa imara zaidi.
Ashanti ipo kwenye mazoezi makali chini ya kocha Mubaraka Hassan kwa ajili ya kujiandaa na ligi daraja la kwanza kwenye uwanja wa Rovers Msimbazi Centre, Ilala.
Akizungumza na BINGWA Katibu wa Ashanti Abubakar Silas alisema kuwa watasajili wachezaji wafungaji (straikers) viungo wa kati (midfield) na mabeki kwani baadhi ya wachezaji wao wamesajiliwa na timu zinazocheza ligi kuu bila kutaja timu.
"Tupo kwenye mikakati ya kufanya usajili na ndio maana unaona wachezaji wapo wengi kwani baadhi ya wachezaji wamesajili na timu za ligi kuu na kuziba nafasi ambazo tuliona zina mapungufu wakati tunacheza ligi ya kituo" alisema Silas.
Vilevile alisema timu ipo vizuri kwani wachezaji wanaomba kusajili wamejitokeza kwa wingi na asilimia kubwa ni wazuri ila tatizo bado analiona kwenye safu ya ushambuliaji.
Pia aliwataka mashabiki kuhudhuria kwa wingi mazoezini ili kusaidia kutoa ushauri kwa uongozi na kocha na si kukaa kimya baadae waanze kulalamika.
"Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi mazoezini ili watoe ushauri kwa kocha na uongozi na kuendeleza mshikamano wetu wa miaka yote", alisema Silas.

Post a Comment