Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 10, 2024

Simba kuanza ligi nyumba, Yanga Ugenini

 

Simba

Yanga

SIMBA na Yanga zinatarajiwa kukutana Oktoba 19, mwaka huu katika mzunguko wa nane wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo ambao ratiba ilitolewa jana, Simba itakuwa mwenyeji ikitumia Uwanja wa KMC, Dar es Salaam na itakutana na Yanga ikiwa na kumbukumbu ya kipigo mara tatu mfululizo, michezo miwili ya Ligi Kuu msimu uliopita na juzi kwenye Ngao ya Jamii.

Aidha, Simba inatarajiwa kuanzia kurusha karata yake ya kwanza ikicheza na Tabora United, Agosti 18 Uwanja wa KMC, Mwenge Dar es Salaam.

Bingwa mtetezi Yanga wataanza kusaka ubingwa wa nne mfufulizo ikicheza na Kagera Sugar ugenini Agosti 29 katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Agosti 16, mwaka huu, wageni kwenye ligi hiyo Pamba Jiji watawakaribisha Tanzania Prisons katika Uwanja wa Kirumba, Mwanza, Agosti 17 Mashujaa wataikaribisha Dodoma Jiji katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma na Namungo dhidi ya Fountain Gate Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Ken Gold itacheza na Singida BS katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya Agosti 18 mwaka huu, JKT Tanzania wataialika Azam FC katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo na Agosti 29, KMC itacheza na Coastal Union.

Mzunguko wa pili utaendelea Agosti 23, mwaka huu na ratiba hiyo yenye timu 16 inatarajiwa kumalizika Mei 24 mwakani.

No comments:

Post a Comment