Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 16, 2018

YANGA YALAZIMISHWA SARE TAIFA LEO
YANGA imeshindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana na Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi wa kombe la Shirikisho la soka Afrika(CAF).
Katika mchezo wa awali Yanga ilibamizwa mabao 4-0 na USM Alger ya Algeria mchezo uliochezwa Algeria wiki mbili zilizopita na hivyo ilihitaji sio zaidi ya ushindi kuweka hai matumaini ya kushika moja ya nafasi mbili za juu.
Kwa upande wa wapinzani wao Rayon hiyo ni sare yao ya pili kwenye mashindano hayo baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Gor Mahia ya Kenya kwenye nchini Rwanda wiki mbili zilizopita na sasa ina pointi mbili huku Yanga yenyewe ikiwa na point moja.
Katika mchezo wa leo Yanga ilikuwa na baadhi ya nyota wake ambao hawakucheza kwenye mchezo uliopita dhidi ya USM Alger ambao ni beki wake mahiri Kelvin Yondani, Obrey Chirwa , Thabani  Kamusoko na Amis Tambwe.
Lakini pia iliendelea kuwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu ambao ni Ibrahim Ajibu na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi anayesumbuliwa na majeruhi.
Ikiwa na baadhi ya nyota wake hao Yanga ilionekana kutulia kwa kiasi fulani hasa katika sehemu ya ulinzi na kiungo ambapo uzoefu wa beki Kelvin Yondani na kiungo Thabani Kamusoko ulionekana kuimarisha kwa kiasi fulani timu hiyo.
Rayon walipata nafasi kadhaa za kufunga katika vipindi vyote viwili lakini washambuliaji wake hawakuwa makini kumalizia nafasi hizo na Yanga kuonekana kucheza vizuri zaidi katika kipindi cha pili cha mchezo huo lakini mshambuliaji kutoka Obrey Chirwa alikosa bao la wazi kwa shuti alilopiga akiwa ndani ya eneo la penalti kugonga  mwamba.
Yanga itakuwa mgeni wa Gor Mahia kwenye muendelezo wa mashindano hayo utakaochezwa Nairobi, Kenya mwishoni mwa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment