Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, January 27, 2018

RUFAA YA DODOMA FC YATUPWA

KAMATI ya saa 72 imetupa malalamiko ya Dodoma FC dhidi ya JKT Oljoro katika mechi iliyochezwa Januari 21, 2018 kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Akizungumza leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi (TPBL) Boniface Wambura alisema malalamiko hayo yalikuwa na sehemu mbili; moja ni uhalali wa mchezaji wa JKT Oljoro, Haki Rubea kuwa hakuwa na leseni, na mbili ni kudai kuwa Mwamuzi na Mwamuzi Msaidizi namba moja walikataa bao lao halali.
“Baada ya kupitia malalamiko hayo, Kamati imebaini kuwa Haki Rubea ni mchezaji wa JKT Oljoro mwenye leseni namba 961111011 iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), hivyo ni mchezaji halali,” alisema Wambura
Pia Wambura alisema kamati haina mamlaka ya kukubali bao ambalo limekataliwa na mwamuzi uwanjani, hivyo kamati imetupa malalamiko ya Dodoma FC kwa hoja zote mbili.
Aidha Wambura alisema kamati imejiridhisha kuwa Kamishna wa mechi hiyo Paul Opiyo na Mwamuzi wa Akiba, Gilbyrth Mrina walifanya makosa kumruhusu mchezaji huyo kucheza bila kuonyesha leseni yake.
Alisema kamati imeteua wajumbe watatu kupitia mkanda wa mechi hiyo ambapo pamoja na mambo mengine itachunguza kiwango cha uchezeshaji cha mwamuzi msaidizi, Emmanuel Muga na mwamuzi wa akiba, Gilbyrth Mrina na kuwasilisha taarifa yake kwa ajili ya hatua zaidi na tayari wameondolewa kwenye ratiba kutokana na kupata maksi chache.
Wakati huo huo timu mbalimbali za daraja la kwanza, viongozi na wachezaji wametozwa faini kutokana na makosa mbalimbali.
Wachezaji wa Friends Rangers Almasi Mkinda na Mtoro Hamisi, wamefungiwa mechi tatu na faini y ash. 300,000 kila mmoja na Prosper Mushi wa African Lyon wamefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000
African Lyon imepigwa faini ya sh. 600,000 baada ya kuonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mechi moja na kugoma kuingia vyumbani, JKT Tanzania imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kuingia eneo la kuchezea kushangilia ushindi
Nayo Polisi Tanzania imepigwa faini ya jumla ya sh. 1,000,000 kutokana na gari la washabiki wa timu hiyo kuingia uwanjani na kuzunguka uwanja wakati timu zikifanya mazoezi na wakati wa mapumziko na baada ya mchezo kumalizika washabiki wa timu hiyo waliwafuata waamuzi na kutaka kuwapiga.

Alliance Schools imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na timu yake kutoingia vyumbani katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 13, 2018 katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma. 

No comments:

Post a Comment