Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 29, 2017

KOCHA NDANDA HANA HOFU NA SIMBA

WAKATI Simba ikitua Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu, Tanzania Bara unaotarajiwa kuchezwa kesho, kocha wa Ndanda FC, Malale Hamsini amesema hana hofu na wachezaji wa kigeni wa Simba.
Akizungumza  Malale alisema anatambua mchezo ni dakika 90 japo mchezo ni mgumu kwa kila upande lakini wamejipanga kwa ajili ya ushindi.
 “Sina hofu na wachezaji wa kigeni wa Simba ninachotambua mchezo wa soka ni dakika 90, hii mechi ni ngumu kila upande kwetu na kwao pia. Tumejipanga kwa ajili ya ushindi na hii sio kwa Simba pekee bali mechi yoyote iliyopo mbele yetu ni kama fainali,” alisema Malale.
Pia Malale aliwataka mashabiki na wanachama wa Ndanda kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao katika mechi hiyo kwani itasaidia kuwapa morali wachezaji kupata ushindi.
Simba iliwasili Mtwara juzi huku Kocha Msaidizi Djuma Masoud akisema ushindi ni muhimu ili kuwapa mashabiki zawadi ya mwaka mpya baada ya kuondolewa kwenye kombe la FA na Green Warriors.
Ndanda haina nyota wa kigeni tofauti na Simba ambao wamesajili nyota wa kigeni akiwemo James Kotei, Laudit Mavugo, Juuko Murshid, Haruna Niyonzama lakini Malale ameonyesha ‘kiburi’ kuwa nyota hao ni wa kawaida kwake.
Katika mchezo huo Simba itawakosa wachezaji Kipa Said Mohamed ‘Nduda’  na Salim Mbonde na Shomari Kapombe ambao ni majeruhi huku beki mpya Asante Kwasi akiachwa Dar es Salaam aendelee kujifua kwa ajili ya mashindano ya Mapinduzi
Kwasi atajiunga na timu itaporejea kutoka Mtwara kwa safari ya Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi ambapo Simba imepangwa Kundi A kwenye Kombe la Mapinduzi pamoja na Azam FC, URA ya Uganda, Jamhuri na Mwenge ambao watafungua nao pazia

Kwa sasa Simba inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 23 baada ya kushuka dimbani mara 11 lakini Azam FC inaweza ikawa kileleni endapo itashinda mchezo wake dhidi ya Stand United.

No comments:

Post a Comment