Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 29, 2017

COWBELL NA MBAO FC WAFUNGA NDOA YA MWAKA MMOJA



MWENENDO mzuri wa Mbao FC umeifanya kampuni ya Hawaii ambao ni wasambazaji wa maziwa ya Cowbell kumwaga milioni 100 kudhamini klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Akizungumza jana Meneja Masoko wa Hawaii Product Supply Ltd Elisaria Ndeta alisema mwenendo mzuri wa Mbao umetushawishi kuendelea kuidhamini na msimu huu dau limeongezeka.
“Msimu uliopita Mbao ndio walituomba udhamini lakini msimu huu sisi ndio tumeomba kuwadhamini na utaona msimu huu dau limeongezeka kutoka sh. milioni 25 hadi sh milioni 100,” alisema Ndeta.
Katika mkataba huo Mbao watakabidhiwa pesa taslimu sh milioni 70  huku sh. milioni 30 zikitolewa kwa njia ya vifaa.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi alisema udhamini huo umekuja wakati muafaka na utaongeza ari ya kuifunga Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuchezwa Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
“Tunaishukuru Cowbell kwa kukubali kuendelea kuidhamni Mbao FC na niwaambie tu kuwa udhamini unaturahisishia maandalizi ya kuifunga Yanga ikiwa ni pamoja na kupandisha morali ya wachezaji,” alisema Njashi.

Cowbell inaungana na kampuni ya GF Trucks & Equipment kuidhamini Mbao FC kama wadhamini binafsi wa timu 

No comments:

Post a Comment