Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 11, 2014

ASHANTI YAPUUZA WANAOWABEZA



 

UONGOZI wa Ashanti United ya Ilala umesema timu yao haiwezi kushuka daraja kwani ina benchi la ufundi makini na wachezaji wenye uwezo.

Akizungumza jijini, Afisa Habari wa timu hiyo, Marijani Rajabu, alisema unawashangaa watu ambao walianza kuiweka timu yao miongoni mwa timu zitakazo zushuka daraja wakati ligi bado haijaanza mzunguko wa pili.

“Mzunguko wa kwanza kweli timu haikufanya vizuri ndio maana uongozi uliliona na kufanya mabadiliko kwenye benchi la uhaijaanza mzunguko wa pili.

“Mzunguko wa kwanza kweli timu haikufanya vizuri ndio maana uongozi uliliona na kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi na kufanya usajili makini na sasa timu imeshavuka mstari wa kushuka daraja”, alisema Marijani

Pia aliwataka mashabiki kuwa wavumilivu pale timu inapofungwa kwani kufungwa mchezo miwili siyo kigezo kuwa timu ni mbovu na kuanza kusema itashuka daraja.

Marijani amesema wamejiandaa vema kuikabili Kagera Sugar kwenye mchezo ujao ambao utachezwa Uwanja wa Chamazi, uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kuwaomba mashabiki kufika kwa wingi kuishangilia timu yao.

No comments:

Post a Comment