Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 11, 2017

UWANJA WA TAIFA KUKABIDHIWA NOVEMBA 24

KAZI ya kukarabati Uwanja wa Taifa inatarajiwa kumalizika Novemba 21 na unakabidhiwa serikalini Novemba 24.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Operesheni SportPesa Luca Neghesti leo wakati kamati ya maandalizi ya fainali za Afrika (afcon U-17) ilipokagua uwanja huo ikiongozwa na Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
“Kazi ya kukarabati sehemu ya kuchezea imekamilika na nyasi zilizooteshwa zimeota vizuri na zimeshika hivyo upo tayari kutumika,” alisema Luca.
Akizungumza Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe aliishukuru SportPesa ambao ndio wanakarabati uwanja huo.
“Nashukuru kuona uwanja nyasi zimeota vizuri na unapendeza na kikubwa nashukuru kwa vijana wetu sita ambao wamefundishwa namna ya kutunza viwanja,” alisema Dk. Mwakyembe.
Pia Mwakyembe alisema vijana sita waliopata mafunzo hayo ni mmoja tu ndio aliyeajiriwa serikali na kuwasihi kuwa wavumilivu wakati wakifanya mchakato wa ajira zao.
Aidha alitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuandaa mchezo wa ligi ambao utachezwa Novemba 24 kwa ajili ya kukabidhiwa uwanja, jambo ambalo Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alisema wataangalia namna ya kupata mchezo kwani inawezekana ratiba ikawa imesimama kupisha Chalenji.

“Tutaangalia kwani leo na kesho tutakuwa na kikao na boodi ya ligi kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya ligi kwani timu za Taifa ya bara na ile ya Zanzibar zitakuwa kwenye mashindano ya Chalenji inayotarajiwa Novemba 25,” alisema Kidao.

No comments:

Post a Comment