Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 11, 2017

MAKONDA NDANI YAKAMATI YA WATU 25 YA KUANDAA FAINALI ZA VIJANA AFRIKA

SERIKALI imeunda kamati ya maandalizi ya fainali za soka za Vijana za Afrika (AFCON U-17) zilinazotarajiwa kufanyika nchini 2019.
Akizungumza leo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Dk. Harrison Mwakyembe alisema kamati hiyo ina watu 25 na imefanya kikao chake cha kwanza leo.
“Tanzania kama nchi tuna mtihani mgumu na mtihani huu ni lazima kufaulu hivyo serikali imeunda kamati ya watu 25 ambayo ndani yake zitapatikana kamati nyingine ndogo ndogo,” alisema Dk. Mwakyembe.
Pia alisema 2019 ipo karibuni ndio maana kikao cha kwanza kilichokaa jana wajumbe walichagua mwenyekiti wa kamati na makamu wake pamoja na mtendaji wa kamati.
“Kamati hiyo, mimi ndio nimechaguliwa kuwa mwenyekiti na Leodgar Tenga amechaguliwa kuwa makamu na mtendaji wa kamati amechaguliwa Henry Tandau na wajumbe wote walioteuliwa wamekubali,” alisema Dk. Mwakyembe.
Wajumbe ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura, Mkuu wa kitivo cha sheria Chuo Kikuu Huria, Dk. Damas Ndumbaro, Dk. Francis Michael  kutoka kitivo cha sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamis Kigwangala, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James,Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna Makakala, Mkurugenzi Mtendaji wa Ngorongoro kreta Dk. Freddy Manongi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mohamed Enterprises Ltd, Mohammed Dewji, Mkurugenzi Mtendaji Said Salim Bakhresa &Co Ltd, Abubakar Bakhresa, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Yusuph Singo.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Wiliam Erio, Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Dk. Lawrance Maseru, Mtendaji Mtendaji wa ATCL, Eng. Ladislaus Matindi, Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi na  Ofisa Masoko Mkuu wa SportPesa, Kelvin Twisa
Mkurungezi wa Manispaa ya Temeke Nassib Mmbagga, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya TFF, Ahmed Mgoyi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Vijana ya TFF, Khalid Abdallah, Angetile Osiah kutoka Mwananchi Communications, Lameck Nyambaya mjumbe wa kamati ya Utendaji TFF.

Tanzania ni mara ya kwanza kuandaa fainali za mashindano ya soka ya Afrika hivyo ni nafasi pekee ambayo inapaswa kutumika vema kwani itaitangaza nchi katika kimataifa katika uchumi, raslimali, na hata kutangaza wachezaji wetu 

No comments:

Post a Comment