Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 29, 2017

Gazza machozi kufikisha miaka 50



Paul Gascoigne
LONDON, England
MKONGWE wa soka wa England, Paul Gascoigne ‘Gazza’ ameangua kilio kutokana na hisia kali, anapofikisha umri wa miaka 50, akisema alihisi hangefika kutokana na ulevi wa kupindukia.
Gazza alikutana na rafiki na wadau wake mbalimbali kwenye hafla ya kutimiza nusu karne hiyo, ambapo pia iliendesha harambee kwa ajili ya kupambana na mzio wa kilevi na uraibu wake.
Anasema kufika umri huo ni hatua kubwa sana, ikizingatiwa jinsi alivyokuwa akiyachapa maji, na kwamba sasa analenga kupambana na hali hiyo, si kwake tu, bali kwa watu wote.
Nyota huyu amekuwa akilinganishwa na mwingine mkubwa, George Best, ambaye kama Gazza, alikuwa mzuri sana enzi za usakataji soka uwanjani, lakini baada ya hapo alikuwa na kashfa za ulevi wa pombe na matumizi ya dawa za kulevya kupindukia.
Katika tawasifu yake, ‘Gazza-My Story’ Mwingereza huyo anasema kwamba tabia yake imemtia matatani, akihangaika na maisha baada ya kumaliza uchezaji soka, akisema kwamba mwaka jana ulikuwa mbaya zaidi katika maisha yake.
Gazza alianzia soka yake Newcastle, akaja kuwa mmoja wa wachezaji wachache kukataa ofa za aliyekuwa Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson, akisema sababu ni kwamba Old Trafford ni kaskazini mno.
Mwaka 1988 aliondoka Newcastle na kujiunga na Tottenham Hotspur na pia akakipiga na Timu ya Taifa ya England – Three Lions.
Mama yake, Caro (72) anasema kwamba mwanawe alihamia Spurs kwa sababu ya msingi, kwamba alikuwa amekorofishana na watu wa benchi la ufundi
la Newcastle.
Klabu nyingine alizochezea ni Lazio, Rangers, Middlesbrough, Everton, Burnley, Gansu Tianmna na Boston.
Alianza kujulikana kwa ulevi akiwa Rangers, ambapo alikuwa akiuchapa mtindi kwa sana nyakati za usiku. Vyombo vya habari vilisimulia sana juu ya ulevi wake kuanzia 2005 baada ya yeye kuachana na soka.
Alipewa kazi ya ukocha Kettering Town, lakini alishindwa kukaa hapo kwa muda mwngi kutokana na tabia yake ya ulevi.

No comments:

Post a Comment