Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, November 12, 2017

TAIFA STARS YAILAZIMISHA BENIN NYUMBANI LEO



TIMU ya Taifa ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Benin katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa utakaochezwa katika dimba la Stade de I’Amitie mjini Cotonou.
Benin ambao walikuwa wamepania kulipiza kipigo cha mabao 4-1 walichopata mwaka 2014 kwenye Uwanja wa Taifa walijikuta wakiambulia sare hiyo ambayo ilitokana na mwamuzi kutokuwa makini.
Bao la Benin lilifungwa dakika ya 32 na nahodha mkongwe Stephane Sessegnon kwa penalti baada ya mwamuzi Ligali Praphiou kuashiria pigo hilo kwa madai kuwa Gadiel wa Taifa Stars ndie ameshika wakati aliyeshika alikuwa mchezaji wao Khaled Adenon.
Maamuzi hayo yalionekana kuwachanga wachezaji wa Taifa Stars lakini walijipanga na kutulia na kucheza mpira na dakika ya 39 Simon Msuva alipiga shuti ambalo lilienda langoni lakini kipa alilipangua vizuri.
Kipindi cha pili Taifa Stars walicheza pasi fupi ambazo zilisaidia kupata bao dakika ya 50 lililofungwa na Elias Maguli kwa kisigino akiunganisha pasi ya Shiza Kichuya.
Kama vile kocha wa Taifa Stars alihitaji kufunga mabao zaidi alimtoa kiungo Rafael Daudi na kuingiza mshambuliaji Mbaraka Yusuf, Shiza Kichuya nafasi yake ikachukuliwa na Ibrahim Ajib, Hamis Abdallah akaingia Jonas Mkude baadae akaumia Mudathir akaingia Nurdin Chona.
Kwa matokeo hayo huenda Tanzania ikapanda katika viwango vya FIFA ambayo hutolewa kila mwezi kwani Benin inashika nafasi ya 79 na Tanzania inashika nafasi ya 136 katika viwango vya Oktoba.
Tanzania; Aishi Manula, Himid Mao, Gardiel Michael, Abdi Banda, Kelvin Yondan, Hamisi Abdallah/Jonas Mkude dk 75, Simon Msuva/Boniphace Maganga dk 85, Mudathir Yahya/Nurdin Chona dk 92, Elias Maguli, Raphael Daudi/Mbaraka Yusuph dk 54 na Shizza Kichuya/Ibrahim Ajib dk 65

Kikosi cha Benin kilikuwa; Fabien Farnole, Rodrigue Fassinou, Khaled Adenon, Cedric Hountonji, David Kiki, Djiman Koukou, Olivier Verdon, Jodel Dossou, Stephane Sessegnon, David Djigla Dossou na Steve Mounie.  

No comments:

Post a Comment