Mkurugenzi
Msaidizi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Leah Kihimbi akimkabidhi Tuzo mshindi wa kipengele cha Mbunifu
Bora wa mwaka wa Swahii Fashio Weeek mwaka huu Kiki Zimba.
Na Mwandishi Wetu
Mbunifu
wa mavazi Kiki Zimba ametunukiwa tuzo ya kuwa mbunifu bora wa mavazi
kwa mwaka huu iliyotolewa katika onesho la mavazi la Swahili Fashion
2014.
Pia
Mwanamitindo wa kimataifa mtanzania aishie Marekani Millen Magese
alishinda tuzo ya mtu mwenye mvuto zaidi nchini ijulikanayo kama
Mercedes – Benz Style Icon of the Year iliyotolewa kwenye tuzo za Swahii
Fashion 2014.
Katika kipengele hicho alikuwa akishindanishwa na akina Nasib Abdul, Diamond Platinum, Mohamed Dewji na Wema Sepetu.
Millen pia alitunukiwa tuzo ya kutambua mchango wake kama mwanadada mwenye mchango mkubwa katika kusaidia jamii yake.
Tuzo
hizo zilizoandaliwa na kampuni ya 361 degree ambayo pia imeandaa onesho
hilo, kulikuwa na utoaji wa tuzo nyingine mbalimbali zilizotolewa kwa
wadau wa mitindo nchini kwa lengo la kutambua mchango wao katika
kuendeleza fani hiyo.
Mbunifu
wa mavazi Martin Kadinda alichaguliwa kuwa mbunifu bora wa mavazi ya
kiume huku Jamila Nyangassa akichaguliwa kuwa mwanamke wa mwaka.
Gazeti
tando (blog) ya Missie Populaar ilichaguliwa kuwa blog bora ya mwaka
huku mbunifu wa mavazi Husna Tandika akitajwa kuwa ndio mbunifu bora
anaechipukia.
Pia
mwandishi wa habari wa kituo cha Eatv Deogratius Kithama alichaguliwa
kuwa mwandishi bora wa mavazi ya kiume, na Albert Manifester
alichaguliwa kuwa mpiga picha bora wa masuala ya Mitindo.
Wengine
walioshinda tuzo ni pamoja na Rehema Samo alietajwa kuwa mrembaji bora
wa mwaka na Irfan Rizwanali kuwa mtaalamu bora wa kuwapendezesha watu
mbalimbali.
Akizungumzia
ushindi wa kuwa mbunifu bora wa mavazi kwa mwaka huu, Kiki Zimba
alisema kuwa ushindi huo unatokana na nia ya dhati katika tasnia hiyo
hasa kwa kujituma kwa hali na mali katika kutengeneza nguo bora zaidi.
“Mwaka
huu nimefanya kazi kubwa zaidi kwa kuwabunia watu mbalimbali hadi
nimeweza kushinda tuzo hii ninaomba na watu wengine wajitokeze zaidi
katika kutuunga mkono wabunifu wa ndani kwa kushona nguo kwetu”alisema
Kiki.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Leah Kihimbi alisema kuwa serikali
itaendelea kusaidia tasnia ya Mitindo nchini huku akiipongeza kampuni ya
361 degree kwa kutimiza miaka saba katika kuandaa onesho hilo la
Swahili Fashion Week.
Swahili
Fashion Week na Tuzo za mwaka 2014 zinaandaliwa na 361 Degrees kwa
usaidizi wa Hotel Sea Cliff, Sea Cliff Court, chini ya udhamini wa EATV,
East Africa Radio, Basata, Baileys, Mercedes-Benz, 2M Media, Tanzania
Printers LTD and Syscorp Media.
No comments:
Post a Comment