Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 14, 2017

PINGAMIZI LIGI YA WANAWAKE NA TIMU ZA TAIFA ZITAKAZOSHIRIKI CECAFA KUTANGAZWA WIKI IJAYO

WAKATI Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, ikitarajiwa kuanza Novemba 26, 2017 katika vituo viwili vya Dar es Salaam na Arusha, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema huu ni wakati wa pingamizi baada ya usajili wa msimu huu kwa timu zote 12, kukamilika juzi.
Akuzungumza na wandishi wa habari leo, Ofisa habari wa TFF Alfred Lucas alisema mwisho wa kupokea pingamizi ni Novemba 17.
“Kipindi cha usajili kilikuwa Oktoba 25 hadi Novemba 12 na kuanzia jana hadi Novemba 17, ni kipindi cha pingamizi hivyo viongozi wa timu wanatakiwa kuwasilisha pingamizi kama yapo,” alisema Lucas
Pia alisema Novemba 18, Kamati ya Sheria itakaa kutoa leseni za wachezaji na Novemba 24, kutakuwa na semina ya viongozi wa klabu, Waamuzi na Makamishna Dar es Salaam.
Wakati huo huo Lucas alisema Vikosi vya timu za soka za Taifa ya Kilimanjaro Heroes na Serengeti boys vitatangwa wiki ijayo kwa ajili ya kuingia kambini kujiandaa na mashindano ya Baraza la michezo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Lucas alisema Kilimanjaro Heroes inajiandaa na ambayo inatarajiwa kufanyika Kenya kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 9 na Serengeti inajiandaa na mashindano kama hayo kwa timu za U-17 ambayo yanatarajiwa kufanyika Rwanda kuanzia Desemba 12-22.

Aidha Taifa Stars ilirejea usiku wa kuamkia jana toka Benin ambapo walikwenda kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na kutoka sare na wachezaji wote wameshaondoka kurudi katika timu zao.

No comments:

Post a Comment