Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 14, 2017

SERENGETI BREWARIES YAIPONGEZA TAIFA STARS

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, wameelezea kuvutiwa na kiwango cha soka kilichoonyeshwa na timu hiyo katika mchezo wake dhidi ya Benin.

Juzi (Jumapili) Taifa Stars ilitoka droo ya goli moja kwa moja katika mchezo wa kirafiki dhidi ya  timu ya taifa ya Benin uliochezwa katika jiji la Porto-Novo nchini Benin

Akiongea jana, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser  Mloka alisema,kiwango cha Taifa Stars kimekuwa kikiridhisha na kutia moyo tangu kampuni hiyo iingia udhamini nayo.

Alisema, ni japo la kutia moyo kwamba tangu SBL itoe udhamini, Taifa Stars haijapoteza mechi yoyote, iwe ni  nyumbani au ugenini.

“Tukirejea kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya Benin, kama Benin wasingepata penati ni wazi kuwa Taifa Stars wangeibuka washindi,” alisema

Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, Taifa Stars walicheza vizuri katika mechi hiyo pamoja na kwamba Benin wako mbele yao katika nafasi za Shikisho la Soka Ulimwenguni  (FIFA). Kwa mujibu wa viwango vya FIFA Benin inashikilia nafasi ya 86 huku Tanzania ikishikilia nafasi ya 136.

Ceaser alisema kukosekana kwa wachezaji muhimu wawili wa Taifa Stars Mbwana Sammata na Thomasi Ulimwengu kutokana na kuwa majeruhi pia kumeathiri matokeo huku akisisitiza kuwa timu inaendelea kuboreka

Mwezi Mei mwaka huu, SBL iliingia mkataba wa mitatu na Shirikisho la Mipira wa Miguu Tanzania (TFF)  wa thamani ya shilingi bilioni 2.1  ambao uliifanya kuwa mdhamini  mkuu wa timu ya taifa -Taifa Stars.

Udhamini huo ni wa mara ya pili kwa SBL kuiunga mkono timu ya taifa baada ya kampuni hiyo kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu ilipoidhamini timu hiyo kati ya mwaka 2008 hadi 2011.

 Uamuzi wa kampuni hiyo wa kuidhamini timu ya taifa unatokana na sera ya SBL ya kusaidia kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo.


No comments:

Post a Comment