Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 14, 2017

RAIS WA TFF WALLACE KARIA AMLILIA DYAMWALE


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Chabanga Hassan Dyamwale (76).

Mbali wa wadhifa huo katika eneo la mpira wa miguu,  pia Dyamwale atakumbukwa zaidi akiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na kwa miaka ya hivi karibu alikuwa Mjumbe wa Kamati huru ya uchaguzi TFF tangu 2004 mpaka 2012.

Hayati Dyamwale aliyezaliwa Juni 01, 1941, aliondoka FAT mwaka 1978, lakini pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Michezo nchini miaka ya mwanzo ya 1980 kabla ya kuhamishiwa Handeni mkoani Tanga kuwa Ofisa Utamaduni, lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere akamrudisha Dar es Salaam.

“Nimeguswa na kifo cha Mzee Chabanga Hassan Dyamwale. Inna Lillah wainaillah Rajauun. Natuma salamu zangu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, majirani na marafiki wa hayati Mzee Dyamwale ambaye nimetaarifiwa kuwa amefariki dunia Agosti 13, mwaka huu kwenye Hospitali ya Muhimbili,” alisema Karia.

“Ni msiba mkubwa kwa wanafamilia ya michezo hususani soka,” amesisitiza Rais Karia na kuomba  familia, ndugu, jamaa, marafiki kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kumpoteza mpendwa Dyamwale.

Rais Karia amesema: “Namfahamu Mzee wetu huyu tangu miaka mingi akiwa mteuliwa kutoka serikalini kushika wadhifa wa utendaji ndani ya FAT wakati ule (Kwa sasa ni TFF), alifanya kazi kwa uhodari mkubwa na uadilifu,” amesema Rais Karia.

Rais Karia amesema kwamba mbali ya kuwa mtendaji ambaye alifanya mabadiliko makubwa katika soka la Tanzania kutoka ligi ya kituo kimoja hadi ligi ya mikondo miwili (nyumbani na ugenini). Taarifa zinasema kwamba alifanya kazi hiyo akiwa kwenye hema.

Pia Rais Karia alimfahamu Mzee Dyamwale alipokuwa Meneja wa Uwanja wa Taifa (sasa Uwanja wa Uhuru) aliyekuwa mtaalamu wa masuala ya ujenzi wa viwanja.

Rais Karia amesema kwamba atambukuka zaidi hayati Dyamwale kwa uhodari wake wa kazi na msimamo kwenye jambo aliloliamini lilileta mafanikio makubwa katika soka la Tanzania.

Kumbukumbu nyingine zinaonesha kuwa Dyamwale ndiye aliyebuni mpango wa watoto kuingia bure uwanjani miaka ya 1980 maarufu yosso.

No comments:

Post a Comment