TIMU ya soka
ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ imeanza mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru
Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana unaotarajiwa
kuchezwa Septemba 2
Elias Maguli
ni mchezaji pekee anayecheza soka nje aliyeanza mazoezi huko nahodha Mbwana
Samatta akitajwa kuwasili alfajiri na kufanya idadi kuwa 16 huku wengine watano
wakitarajiwa kuwasili leo.
Katika
mazoezi yaliyofanyika jana kocha Ami Ninje wa Zanzibar ambaye anafanya shughuli
zake nchini Uingereza alikuwa miongoni mwa benchi la ufundi linaloongozwa na
Salum Mayanga.
Ami
alifundisha sehemu ya pili ya mazoezi ya uwanjani baada ya sehemu ya kwanza ya
kupashwa mwili joto kufanywa na kocha msaidizi Fulgence Novatus na sehemu ya
tatu iliendeshwa na kocha mkuu Salum Mayanga.
Akizungumza
kando ya mazoezi hayo, Mayanga alisema baada ya wachezaji kuingia kambini juzi
walifanyiwa vipimo vya afya na na kusema wachezaji wanaocheza nje wanatarajiwa
kuwasili jana usiku.
“Wachezaji
wako fiti ni kama unavyowaona wanafanya mazoezi na morali ipo juu kuikabili
Botswana, kesho (leo) natarajiwa wachezaji wanaocheza soka nje watakuwepo,” alisema
Mayanga.
Lucas
amesema wamekwishafanya mawasiliano na wachezaji wanaocheza nje walioitwa
kujiunga na kikosi cha Stars akiwemo Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili ni Farid
Mussa, Simon Msuva, Hamisi Abdalla, Ergenes Mollel na Abdi Banda.
Wakati huo
huo Ofisa habari wa TFF Alfred Lucas alisema msafara wa wachezaji 18 na
viongozi tisa kutoka Botswana unatarajiwa kuwasili kesho na Ijumaa watafanya
mazoezi katika uwanja wa Uhuru
“Tumewasiliana na Botswana na wamesema
watakuja na msafara wa watu 27 ambao ni wachezaji 18 na viongozi tisa,” alisema
Lucas.
Mchezo huu ni kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka la dunia ambayo huchezwa kila mwezi.
Mchezo huu ni kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka la dunia ambayo huchezwa kila mwezi.
No comments:
Post a Comment