Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 7, 2017

ALI KIBA AMKARISHA AJIB YANGA 
MSANII wa Bongofleva Ali Kiba ‘King Kiba’ amefurahi mshambuliaji Ibrahim Ajib kusajiliwa Yanga na kuahidi kumpa ushirikiano japo amekiri kutomfahamu vizuri.
Akizungumza na gazeti hili, Ali Kiba ambaye ni shabiki wa Yanga alisema kila walipokuwa wanakwenda uwanjani kutazama mechi za Simba na Yanga watu wanaomfahamu vizuri Ajib ndio walikua wakimuonesha kwamba yule ndio Ajib.
“Ninasikia ni mchezaji mzuri na ana kipaji kikubwa, watu wanazungumza, wanampigania, wanalalamika kwani mchango wake unaonekana ulikuwa mkubwa Simba hivyo amekuja Yanga, namkaribisha na nitamsapoti,” alisema Ali Kiba
Ajib alitambulishwa juzi na kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Yanga baada ya mkataba wake na Simba kumalizika
Ajibu mwenye uwezo wa kufumania nyavu kama mshambuliaji wa kati , mchezeshaji wa juu anakwenda kukutana na safu tishio ligi kuu kwa ufungaji ya Donald Ngoma, Amisi Tambwe na Simon Msuva.

No comments:

Post a Comment