Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 7, 2017

ZENA CHANDE AAHIDI MAKUBWA SOKA LA WANAWAKE Image may contain: 1 person, smiling, closeup
MGOMBEA Zena Chande wa nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Shirikisho la Soka (TFF) katika uchaguzi wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), unatarajiwa  kutafanyika kesho Dar es Salaam amesema endapo atachaguliwa tena atahakikisha wanaendeleza soka na kuboresha.
Zena ambae ni mhariri msaidizi wa michezo wa gazeti hili alisema kwa kushirikiana na wenzake wataboresha soka katika kipindi cha miaka minee ambacho watakaa madarakani.
“Uongozi wetu tumeanzisha ligi kuu ya wanawake na Taifa cup ya wanawake hivyo tukipewa ridhaa na wajumbe tutashirikiana kuboresha pale tulipoishia ili ligi kuu iwe na timu kila mkoa,” alisema Zena.
Mkutano Mkuu wa TWFA unatarajiwa kufanyika Dar es Salaam na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali waliwasili juzi na jana.
Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba, alisema taratibu zote zimekamilika na kinachosubiriwa na wajumbe kuingia kwenye ukumbi kusikiliza sera za wagombea na kupiga kura.
Tayari Kamati ya Mushumba ilitangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi  huo ambao ni Amina Karuma (Mwenyekiti), Rose Kisiwa (Makamu Mwenyekiti), Somoe Ng’itu (Katibu Mkuu), Theresia Mung’ong’o (Katibu Msaidizi), Hilda Masanche (Mwekahazina),
Wengine ni Zena Chande na Salma Wajeso (Mkutano Mkuu wa TFF)  Mwamvita Kiyogoma, Triphonia Temba, Jasmine Soudy na Chichi Mwidege (wajumbe wa kamati ya utendaji)