Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 7, 2017

TELELA ASEMA SHULE KWANZA USAJILI BAADAE



 Image result for TELELA
KIUNGO mshambuliaji wa Ndanda FC ya Mtwara, Salum Telela ‘Abo Master’ amesema haumizi kichwa kuhusu usajili unaoendelea badala yake amejikita katika masomo.
Telela anayesomea Shahada ya Uhasibu mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Saut tawi la Mtwara, alisema amepokea ofa nyingi kutoka timu mbalimbali nchini lakini akili yake ipo zaidi kwenye kitabu kwa sasa.
Kiungo huyo wa zamani wa Yanga alisema hana uhakika kama ataendelea kuchezea Ndanda msimu ujao au la kutokana na timu nyingi kuonyesha nia ya kuhitaji saini yake lakini bado hakuna aliyofikia nayo makubaliano.
“Sifikirii sana nitakuwa wapi msimu ujao, nimejikita kwenye masomo zaidi japokuwa nimepokea ofa nyingi kutoka timu mbalimbali ila sio kipaumbele changu ila nitakayokubaliana nayo maslahi nitajiunga nayo,” alisema Telela.
Timu mbalimbali zinaendelea kuimarisha vikosi vyao kwa kusajili wachezaji wanaoamini wataweza kuwasaidia kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi baadae mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment