Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 1, 2017

ZILIZOPANDA LIGI KUU ENGLAND MSIMU UJAO HADHARANIHATIMAYE watatu wa kupanda Ligi Kuu ya England (EPL) wamekamilika baada ya Huddersfield kuingia, huku wakiwa na mpango madhubuti wa kukabiliana na vigogo hapo, na wala si kuingia tu kwa maana ya ushiriki.
Walifanikisha kazi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa – Wembley, ambako ndio kwa kawaida huchezwa mechi kubwa za kitaifa kama za kupata wanaoingia EPL, fainali za Kombe la FA, Kombe la Ligi, pamoja na mechi za Timu ya Taifa ya England – Three Lions.
Hii ni mara ya kwanza kwa Huddersfield wanaofundishwa na David Wagner kuingia ligi kuu, ambapo maelfu ya washabiki wake waliingia mitaani Reading kwa ajili ya kushangilia timu ilipopita kwenye basi kubwa la wazi.
Wanaungana na Newcastle United wa Rafa Benitez na Brighton & Hove Albion kwenye kimbembe cha EPL msimu ujao. Hii ni klabu ambayo shabiki wake mkubwa ni Waziri Mkuu wa zamani, Harold Wilson.
Hali haikuwa ya kawaida kwenye St George’s Square — lisilohusishwa kwa miaka mingi na maandamano ya kupongeza timu kama hivi, lakini sasa kuna mwamko mpya na burudani, kama ilivyokuwa Leicester, pale klabu hiyo walipotwaa ubingwa wa England pasipo kutarajiwa.
Klabu tatu hizi zinachukua nafasi zilizoachwa na Hull, Middlesbrough na Sunderland walioshindwa kuhimili mnyukano kwenye ligi kubwa zaidi nchini England na maarufu zaidi duniani iliyoshuhudia Chelsea wakitwaa ubingwa.