Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 1, 2017

Bale aitangazia ubaya Juventus


Related image
WAKATI Real Madrid wakijiandaa kuumana na Juventus kwenye fainali ya kukata na shoka ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) Jumamosi hii nyumbani kwa Gareth Bale jijini Cardiff, mchezaji huyo ameng’aka na kusema hali ni mbaya na UCL haijapata kuacha waliomo salama.
Bale aliyepata kuwa mchezaji ghali zaidi duniani, akiuzwa Madrid kutoka Tottenham Hotspur kabla ya kuja kuzidiwa na Paul Pogba aliyeuzwa kwa pauni milioni 89 kutoka huko Juventus kwenda Manchester United, anasema anapiga hesabu jinsi ya kuwamaliza Wataliano hao.
Nyota wa Madrid wanajifua, wakiamini kwamba watafanya vyema, hasa baada ya Bale aliyekuwa majeruhi kurejea uwanjani, japokuwa mwenyewe anasema kwamba hajakuwa timamu kwa asilimia 100. Anatarajiwa kuungisha nguvu pale mbele na Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.
Japokuwa atakuwa anacheza jijini kwake Cardiff, Bale anasema mambo hayo ufanye kuyasikia tu kwa watu lakini ukishaingia ndani mwake, kuna kuachwa mpauko au kushinda, na hakuna kubaki bila upande – ni kupiga au kupigwa tu.
Upo uwezekano mkubwa kwa mchezaji huyu wa kimataifa wa Wales kuanzia benchi lakini akaingia baada ya muda, akiwa ameanza mechi 23 kwenye mashindano yote msimu huu. Kocha Zinedine Zidane hana shaka kwamba ataweza kupanga watu wanaoweza kumpa matokeo chanya kwenye mechi hiyo.
“Sipo timamu kwa asilimia 100, nimecheza kwa wiki sita au saba tu. Kudumu dimbani kwa dakika 90 ni ngumu kwangu kwa sababu sijacheza sana soka tangu nilipofanyiwa upasuaji na kuna wakati nilicheza na maumivu makubwa na hata niliporejea nilikuwa nameza dawa. Wiki chache zilizopita zimeniwezesha kupumzisha enka yangu kwa muda,” anasema Bale.

No comments:

Post a Comment