Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, June 1, 2017

Wenger kubaki Arsenal ni kufurahia njaa?



YAMETOLEWA maoni tofauti baada ya uamuzi wa kubaki klabuni Arsenal kwa kocha wao, Arsene Wenger, baada ya msimu uliowatupa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) kwa mara ya kwanza tangu miongo miwili.
Wakati wachezaji kadhaa wa zamani wa Arsenal kama Ian Wright na David Seaman wakiona kwamba kuondoka kwa Mfaransa huyo kingekuwa kiama kwa timu, wapo wengine wanaosema kumbakisha ni sawa na kufurahia njaa na kuifanya iwe endelevu.
Mchambuzi wa masuala ya soka, Gary Lineker anadai kwamba Wenger anajiona kwamba amefanikiwa sana Arsenal, lakini ukweli ni kwamba yupo nyuma sana akilinganishwa na wapinzani wake wakubwa kwenye Ligi Kuu ya England (EPL).
Lineker ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa England anakwenda mbali zaidi akionesha uchuro, ambapo anasema uwezekano mkubwa ni kushindwa tena kufuzu kwa UCL msimu ujao kwa sababu hawezi kupata wachezaji matata kuliko klabu nne zilizo juu yake na pia baadhi za chini, kama Manchester United.
Wenger amekubali mwito wa mmiliki wa klabu hiyo, Stan Kroenke, na kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuanzia kiangazi hiki, wakati baadhi ya washabiki na wadau wa Arsenal walitaka mabadiliko kwa kuwa na kocha mpya wakati huu.
Lineker anaungwa mkono na golikipa wa zamani wa Arsenal, Bob Wilson anayesema anachokiona ni ugumu kwa klabu hiyo ya London Kaskazini kuvutia wachezaji wa hadhi ya juu.
“Unawezaje, kwa mfano kumpata mtu kama Antoine Greizmann aje hapo kusaini mkataba? Bila kuwa kwenye michuano ya UCL njia pekee unayoweza kuwavutia wachezaji wakubwa ni kuwalipa mishahara mikubwa,” anasema, ikijulikana jinsi Wenger asivyopenda kutoa mishahara minono.
Anatoa mfano wa Chelsea walivyomsajili N’Golo Kante kiangazi kilichopita licha ya kumaliza chini ya Arsenal, huku The Gunners nao wakitaka kumsajili kutoka Leicester lakini akakataa kwa sababu ofa yao ya mshahara ilikuwa chini sana na hata wakiwa UCL kwake haikuwa na maana.
“Bodi ya Wakurugenzi ya Arsenal ilitakiwa kutazama mambo katika uhalisia wake, ijiulize iwapo katika mazingira haya watashindana kweli? Hawawezi kuchuana na Manchester City wala Chelsea kwa fedha yote ambayo Roman Abramovich na Sheikh Mansour walizo nazo na wanazolenga kuwekeza kwenye klabu zao.
Wachambuzi wanajiuliza iwapo Wenger anaweza tena kwa sasa kuleta mabadiliko Arsenal, akiwa amekaa kwa miaka 21, akawa na wachezaji tofauti 162 katika muda huo na kutumia pauni milioni 700 kwao. Lineker anasema Arsenal wapo nyuma kuliko Wenger anavyodhani na daima akiwa hapo atakuwa chini ya shinikizo.
Kroenke alikutana na Wenger Jumatatu, wakakubaliana mambo kisha uamuzi huo ukapelekwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi, kama kutimiza tu wajibu, kwa sababu Kroenke mwenye hisa asilimia takriban 70 ndiye mwenye usemi na anayemfuatia, Alisher Usmanov amefungiwa nje ya bodi hiyo.
Hata hivyo, Kocha wa cheslea, Antonio Conte amemtaja Wenger kuwa kocha bora zaidi katika historia hapo.

No comments:

Post a Comment