Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 4, 2017

SERENGETI BOYS YAKWAA KISIKI CAMEROON


WENYEJI wa taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, ‘Serengeti Boys’ timu ya Cameroon juzi walilipiza kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa mjini Yaounde, Cameroon.
Awali Aprili 30, Serengeti boys iliifunga Cameroon 1-0 katika mchezo mwingine wa kujipima nguvu.
Akizungumza na gazeti hili Kocha Mkuu wa Serengeti boys, Bakari Shime alisema katika mchezo huo licha ya kufungwa walicheza vizuri.
“Soka ni mchezo wa makosa, wenzetu waliingia wakiwa wamekamia kulipa kisasi lakini pamoja na kupoteza mchezo, wachezaji walicheza vizuri,” alisema Shime maarufu kama mchawi mweusi.
Pia Shime alisema huo ndio mchezo wa mwisho wa kirafiki zaidi watakuwa wanaendelea na programu za mazoezi ya kawaida.
Serengeti Boys ipo Younde, Cameroon tangu wiki iliyopita ikitokea Morocco ambako iliweka kambi na kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Gabon na kushinda 2-1 kila mchezo.
Serengeti boys inarajiwa kuwasili Gabon Mei 7 ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola na Cameroon imepangwa kundi A lenye timu za wenyeji, Gabon, Guinea na Ghana. 
Itafungua dimba na bingwa mtetezi Mali Mei 15 mjini Libreville Gabon ambako kundi B litakuwa likicheza.