Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 4, 2017

BAADA YA ALIKIBA, BENPAL, MO NA HASHIM THABEET WILDAID YAPIGA HODI SERENGETI BOYS




SHIRIKA la Kimataifa la kulinda wanyamapori la WildAid limeingia makubaliano na Shirikisho  la Soka  Tanzania (TFF) kwa ajili ya kuifadhili timu ya Taifa ya Vijana miaka 17, ‘Serengeti Boys’.
Akizungumza wakati wa kuweka saini makubaliano hayo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi alisema wamefurahi kufanya kazi za kijamii hasa hii ya kupiga vita ujangili dhidi ya wanyama pori.
 “Utunzaji mbaya wa mazingira unafanya wanyama kukimbia maeneo yao ya asili na ujangili unamaliza wanyama hasa Tembo hivyo kupitia Serengeti boys tutakuwa na nafasi ya kueleimisha jamii juu ya kuifadhi wanyama na mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo,” alisema Malinzi.
Upande wa jamii tunapenda kushirikiana na jamii kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa jamii huku akitolea mfano kick aids na kujikinga na malaria ambayo ilitekelezwa kipindi cha Tenga.
Naye Mshauri wa WildAid Tanzania Lily Massa alisema anashukuru kufanya kazi na TFF kwa sababu mchezo wa soka unapendwa na watu wengi hivyo watakuwa wanaelimisha umuhimu wa WildAid.
“Nafurahi kufanya kazi na TFF kwani unabeba idadi kuwa ya watu kwa wakati mmoja hivyo elimu kuhusu ujangili na utunzani wa wanyama pori na mazingira itafika kwa jamii,” alisema Lily
WildAid tayari inafanya kazi na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet anayecheza Marekani na mwanamuziki Ali Kiba, BenPal na mfanyabiashara Mohamed Dewj ‘MO’ hivyo kuongezeka kwa TFF kunafanya wafikie watu wengi.

No comments:

Post a Comment