Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 3, 2017

CHAMELEONE NA MKEWE BADO WAPO WAPO SANA
MWANAMUZIKI Jose Chameleone kutoka nchini Uganda ameziondoa tetesi za kutengana na mkewe baada ya wawili hao kuonekana wakiwa pamoja katika sherehe ya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.
Mwimbaji huyo wa ‘Sweet Banana’ alivipamba vichwa vya habari katika siku za hivi karibuni baada ya mkewe Daniella Atim kuripotiwa kwenda mahakamani kudai talaka, lakini wawili hao wameonekana wakiwa pamoja katika sherehe hiyo.
Daniella aliripotiwa kumshitaki Chameleone kwa kumnyanyasa, kurudi nyumbani usiku amelewa, kumpiga bila sababu na alishindwa kuendelea tena na ndoa yenye manyanyaso hadi kufikia hatua ya kwenda Mahakamani kwa ajili ya kuivunja.
Mtandao wa BIGEYE umeripoti kuwa pamoja na kutokea matukio hayo msanii huyo ameahidi kubadilika na Daniella ameamua kurudi nyumbani baada ya kuondoka na kwenda kuishi mbali na mumewe kwa takribani mwezi mmoja.

Wawili hao walionekana wakiwa wameziondoa tofauti zao na kuonyesha mapenzi kama ilivyokuwa siku za nyuma. Chameleone na Daniella walishikana mikono wakati msanii huyo akisherehekea miaka 39 ya kuzaliwa kwenye Lounge ya Cayenne Jumapili.
Kamera ziliwanasa wakiingia ukumbini wakiwa wameshikana mikono usiku mnene huku wakiwa karibu kwa muda wote ambapo Chameleone alikuwa akisherehekea siku yake kubwa na marafiki wake wa karibu, familia na mashabiki. Walionekana wakifurahi pamoja kwa muda wote wa sherehe hiyo iliyomalizika asubuhi.