Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, April 2, 2017

SAMATTA AENDELEA KUTAKATA UEFA EUROPA LEAGUE
 
MSHAMBULIAJI  wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta juzi aliifungia bao moja timu yake, KRC Genk ikishinda 4-0 Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk dhidi ya Lokeren .
Samatta alifunga bao lake dakika ya 72 katika mchezo wa mchujo wa kuwania kucheza UEFA Europa League msimu ujao.
Mabao mengine ya Genk yalifungwa na Alejandro Pozuelo dakika ya 45, Jean-Paul Boetius kufunga la tatu dakika ya 77 na Jose Naranjo kumalizia la nne dakika ya 90.
Bao hilo linamfanya Samatta mabao 18 katika mechi 49 alizochezea Genk tangu asajiliwe Januari 2016 , akitokea TP Mazembe ya DRC huku akiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao mawili aliyofungia timu ya Taifa, Taifa Stars dhidi ya Botswana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Machi 25.
Genk inaongoza Kundi B lenye timu sita ikiwa na pointi 3 sawa na Kortrijk huku timu zote zikiwa zimecheza mechi moja lakini Genk inaongoza kwa tofauti ya wastani wa mabao mengi.