Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, April 2, 2017

HIMID AOMBA RADHI KWA ZULU
KIUNGO wa Azam FC Himid Mao amemuomba radhi kiungo wa Yanga, Justine Zulu baada ya kumuumiza mguu wakati wa mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Taifa jana na kumsababisha kushindwa kuendelea na mchezo.
Zulu aliumia dakika ya 31 na kutolewa uwanjani kwa machela na kupelekwa moja kwa moja kwenye zahanati ya uwanjani ambapo alishonwa nyuzi tisa.
Himid ameonyesha kujutia rafu hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter akisikitishwa na tukio hilo ambalo amesema alilitenda bila kukusudia.
“Nampa pole mchezaji Justine Zulu kwa kuumia, haikuwa nia yangu kumuumiza ni bahati mbaya, nilienda kumpa pole wakati wa mapumziko,” aliandika Himid kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Zulu anatarajiwa kukaa nje kwa kipindi kisichopungua wiki mbili, kufuatia kuumia ugoko wa mguu wa kushoto
Akizungumza na gazeti hili daktari huyo wa tiba za wanamichezo, Nassoro Matuzya alisema Zulu atakuwa nje kwa muda usiopungia wiki mbili.
“Atakaa na nyuzi kwa muda wa wiki moja na baada ya hapo atahitaji wiki moja ili jeraha lake lipone vizuri baada ya hapo anaweza kuanza mazoezi mepesi,”alisema Matuzya.
Hii ni mara ya pili kwa Himid kumfanyia rafu na kumweka nje muda mrefu Zulu baada ya Januari kumchezea rafu kwenye mchezo wa kombe la Mapinduzi na kukaa nje wiki tatu. 
Kuumia kwa Zulu kunaongeza idadi ya majeruhi Yanga kuwa wanne, ambao ni kiungo Thabani Kamusoko, washambuliaji Donald Ngoma na Amissi Tambwe.