Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 16, 2017

YANGA YAENDA ZAMBIA BILA WASHAMBULIAJITambwe Klabu ya Yanga inatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco.
Kikosi cha wachezaji 20 kinatarajiwa kuondoka kwa ndege ya Shirika la Kenya kwenda Lusaka kucheza mchezo huo utakaopigwa siku ya Jumamosi.
Hata hivyo, kikosi hicho cha Mzambia, George Lwandamina kitawakosa wachezaji wake tegemeo katika safu ya ushambuliaji ambao wana udhuru tofauti.
Washambuliaji asilia wote, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Malimi Busungu na Matheo Anthony wataukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali kubwa ikiwa majeruhi.
Matumaini ya Yanga inayohitaji angalau sare ya mabao 2-2 kufuzu hatua ya makundi sasa inabakia kwa viungo washambuliaji Obrey Chirwa na Simon Msuva.
Kocha Lwandamina atalazimika kumuanzisha mshambuliaji Emmanuel Martin aliyeingia kipindi cha pili katika pambano la kwanza.
Mwaka jana, Yangaa ilienda Angola bila Donald Ngoma na Thaban Kamusoko  waliokuwa wakitumikia adhabu za kadi na kupata matokeo yaliyoivusha hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho.