Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 16, 2017

WATANZANIA WAPEWA NAMBA YA KUCHANGIA SERENGETI BOYS




KATIKA kuhakikisha watanzania wanapata hamasa ya kuishangilia timu ya Taifa ya soka ya Tanzania U-17, ‘Serengeti Boys’ wanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ na Ali ‘King’ Kiba watarekodi wimbo maalum wa kuhamasisha kampeni za kuchangia timu hiyo kuelekea Gabon.
Serengeti boys ambayo imefuzu fainali za vijana za Afrika zitakazofanyika kwenye mji wa Librazaville, Gabon inahitaji bilioni moja kwa ajili ya kushiriki fainali hizo zinazotarajiwa kuanza Mei 14 ambayo ipo kundi moja na Mali, Niger na
Akizungumza na wandishi wa habari jana Mwenyekiti wa Kamati ya hamasa ya Serengeti boys ambayo ipo chini ya serikali, Charles Hilary alisema wameweka mikakati ya kukusanya fedha kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo.
“Tuliteuliwa mwezi uliopita na ni muda mfupi sana kabla ya mashindano kuanza lakini tumekutana na tumeweka mikakati ya kupata kiasi cha bilioni moja na kauli mbiu ni ‘Kutoka Gabon kwenda India kwenye fainali za dunia’, “ alisema Hillary.
Hillary alisema msaada wanaohitaji siyo pesa tu hasa msaada wa vyakula, usafiri wa ndege na vifaa kwa ajili ya kambi kwani itakwenda kuweka kambi Morocco.
Aidha alisema njia ambazo wameoanisha kupata pesa ni kupitia kila halmashauri kuchangia kiasi cha milioni moja kila moja na namba ya simu ambayo kila mtanzania anaweza kuweka pesa na kupiga akachangia.
“Kila mtanzania anaweza kuchangia kuanzia shilingi 500 na kwa kuzingatia wingi wa watanzania tutakuwa tumepata pesa za kutosha nap engine kubaki kwa ajili ya kuipeleka timu hiyo India kwani tunaamini tutafuzu,” alisema Hillary.
Pia Hillary alisema kiwanda cha bia cha Serengeti na Mamlaka za hifadhi za Taifa (TANAPA) wameonesha nia ya kushirikiana na kamati kutokana na jina la timu hiyo kufanana moja ya bidhaa/huduma zao.
Naye mjumbe wa kamati hiyo, Beatrice Singano alisema unapiga namba 223344 na kulipia Selcom na unaweza kulipia kupitia mitandao ya Airtel, Vodacom na Tigo.
“Ukipiga namba 223344 unakwenda kwenye namba ya mtandao unaotumia halafu unachagua Selcom na kuweka kiasi cha fedha ambazo unachangia na pia unaweza kuweka kiasi chochote unachopenda,” alisema Singano
Naye mjumbe Maulid Kitenge alisema tayari ala za wimbo ambao utaimbwa na Ally Kiba na Diamond kwa kushirikiana na wasanii kama Mwasiti, Darassa, Vanessa Mdee na Msagasumu ikwishatengenezwa na wasanii  wametumiwa kwa ajili ya kuingiza sauti.
 “Ali Kiba yuko Marekani lakini amekwishatumiwa ala ili aingize sauti ila Diamond yupo nchini na ametumiwa ala na wameahidi kufanya hivyo mara moja na kurejesha kazi hizo, ili na wasanii wengine waingize sauti zao,”amesema Kitenge.
Wimbo huo utakapokamilika watanzania wanaweza kuununua kama ringtone kwenye simu zao pia utasambaza kwenye vyombo vyote vya habari kwa ajili ya kupigwa kuhamasisha watanzania.
Ally Kiba na Diamond wapo kwenye Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ya kuhamasisha na kuwaunganisha watanzania kuichangia Serengeti Boys ambayo ilifuzu fainali za Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14,  mwaka huu.
Wajumbe wengine ni Selestine Mwesigwa ambaye ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Maulid Kitenge wa EFM Radio na TV, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano na Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu.
Wengine ni Mkurugenzi wa Habari, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas; Mkurugenzi wa Global Publishers Limited, Eric Shigongo na Mkurugenzi wa Radio Clouds, Ruge Mutahaba.


No comments:

Post a Comment