Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 17, 2017

SERIKALI YAPONGEZA ZANZIBAR YAAHIDI USHIRIKIANO FIFA






SERIKALI ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na ile ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimepongeza hatua ya Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kupata uanachama wa kudumu katika Shirikisho la Soka Afrika (CAF)
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Rashid Ali Juma alisema anashukuru ushirikiano wa Serikali ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri Nape kwa kusimamia  na kuhakikisha ZFA Inapata uanchama CAF.
“Nashukuru Zanzibar kukubalika na kupata mwanacham kamili wa CAF majira ya saa 6.45 mchana kwani umefika wakati sasa kuona bendera ya Zanzibar, wimbo wa Taifa wa Zanzibar ukipigwa wakati wa mashindano ya kimataifa,” alisema Juma.
Aidha Juma alisema Wanzazibar wanatakiwa kutekeleza kwa vitendo kile ambacho walikuwa wanalilia kuonesha vipaji ambavyo walikuwa wanasema hawapati nafasi ya kutosha na kuahidi ushirikiano kwa ZFA kupata katiba nzuri kuendana na matakwa ya CECAFA na CAF ili iwe njia rahisi ya kupata uanachama wa FIFA.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya  Michezo wa Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Yusuph Singo, alipongeza juhudi za Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kuhakikisha Zanzibar imepata uanachama wa CAF kwani haikuwa kazi rahisi na kuahidi ushirikiano zaidi kwa TFF na ZFA.
“Zanzibar kupata uanachama wa CAF ni hatua mojawapo ya kuanza kuomba pia kuwa mwanachama wa FIFA hivyo nawahakikishia ushirikiano kuhakikisha tunapiga hodi Zurich kuomba uanachama,” alisema Dkt. Singo.
Aidha Dkt Singo alisema moja ya sifa ya kuwa mwanachama wa FIFA lazima uwe mwanachama wa shirikisho la Soka katika bara unalotoka, kwa sasa Zanzibar ina sifa ya kuwa mwanachama  wa fifa na utaratibu wa kuomba unataanza mara moja.
Naye Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Jamal Malinzi alisema furaha ya kuona Zanzibar akiwa mwanachama hawezi kuieleza kwani ni jambo ambalo lilikuwa linamhuzinisha kuona wanakataliwa uanachama.
“Leo tunasheherekea Zanzibar kuwa mwanachama furaha ambayo siwezi kuilezea lakini tulipambana na hatimaye tumefanikiwa na kuhusu wachezaji wanaotoka Zanzibar ni swala la kikanuni ambalo tutalifanyia kazi watanzania wasubiri wakati kanuni zikiandaliwa,” alisema Malinzi
Kwa upande wa mjumbe wa heshima wa Shirikisho la Soka Barani Afrika, Said Elmaamry alisema ana furaha baada ya Zanzibar kupata uanchama kwani ni kazi ambayo wameipigania kwa kipindi kirefu ingekuwa watu wengine wangekuwa wamekata tamaa.
“Tusahau yaliyopita kwani kuna mataifa ambayo yalikuwa hayataki Zanzibar ipate wanachama wakihofia kuwa sisi ni ndugu tutaachiana kwenye mashindano ya kimataifa lakini Bara tunatakiwa tujue tunapocheza na Zanzibar ni timu mbili tofauti wasishangae wakiona Zanzibar wanaonesha ushindani,” alisema Elmaamry
Zanzibar imekuwa nchi ya 55 kupata uanachama juzi kwenye Mkutano Mkuu wa Caf uliofanyika Ethiopia ambapo Hamad Hamad wa Chama cha Soka cha Madagascar alichaguliwa kuwa  Rais na kumwangusha Issa Hayatou aliyedumu tangu 1988.

No comments:

Post a Comment