Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, March 1, 2017

WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA YANGA NA AZAM MASHINDANO YA AFRIKA HADHARANI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limeteua waamuzi wanne wa Tanzania watakaokwenda kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya timu za A Porto Louis 2000 ya Mauritius na El Hilal ya Sudan wikiendi ijayo.

Katika mchezo huo ambao utafanyika ama Machi 17, 18 au 19 Mwamuzi wa kati atakuwa Israel Mujuni Nkongo wakati wasaidizi wake watakuwa ni Samuel Hudson Mpenzu na Josephat  Bulali huku Mwamuzi wa akiba akiwa ni Elly Ally Sasii.

Kamisha katika mchezo huo Na. 78 atakuwa Jerome Kelvyn Damon kutoka Afrika Kusini.

Wakati huo huo, waamuzi watakaochezesha mchezo kati ya Young Africans ya Tanzania na Zanaco FC ya Zambia wamefahamika. Waamuzi kutoka Djibouti ni Djamal Aden Abdi ambaye atapuliza kipenga wakati wasaidizi wake ni Hassan Yacin na Farhan Salime ilihali mwamuzi wa akiba atakuwa Souleiman Djamal.

Kamishna katika mchezo huo Na. 61 atakuwa Luleseged Asfaw kutoka Ethiopia.

Pia CAF imetanga waamuzi watakochezesha mchezo kati ya Azam FC ya Tanzania na Mbabane Swallows ya Swazland. Mchezo huo wa kuwania Kombe la Shirikisho utachezeshwa na waamuzi kutoka nchi ya Benin.
Mwamuzi wa kati atakuwa Addissa Abdul Ligali wakati wasaidizi wake watakuwa Medegnonwa Romains Agbodjogbe na Babadjide Bienvenu Dina huku Mwamuzi wa akiba akiwa Moumouni Kiagou na kamisha wa mchezo atakuwa Mohamed Omar Yusud wa Kenya.

No comments:

Post a Comment