WAWAKILISHI
wa Tanzania katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika Yanga, leo
walishindwa kutoka na karamu ya mabao baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na
Ngaya na Comoro kwenye Uwanja wa Taifa.
Mashabiki wa
soka nchini walitarajia ushindi wa mabao mengi kutoka kwa Yanga hasa
ukizingatia kuwa timu hiyo ilipata mabao 5-1 katika mchezo wa kwanza
uliofanyika Moroni wikiendi iliyopita.
Yanga sasa
imesonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 6-2 na kuisubiri ama Zanaco ya
Zambia au APR ya Rwanda, ambazo nazo zilikuwa zikicheza jana Kigali.
Katika
mchezo wa jana, Ngaya ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Yanga baada
ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 19 lililofungwa na Zamir Mohamed
baada ya shuti kumbabatiza Bossou na kumpoteza kipa Deogratius Munish na kujaa
wavuni.
Yanga
walisawazisha dakika mbili kabla ya mapumziko kwa bao la Hajj Mwinyi aliyepiga
shuti kali la mbali lililokwenda moja kwa moja wavuni.
Awali,
dakika nne tangu kuanza kwa mchezo, Yanga walikosa bao baada ya Emmanuel
Martine kushindwa kuunganisha wavuni mpira wa krosi uliopigwa na Juma Abdul.
Martine
alikosa bao tena dakika nane baadae kufutia krosi ya Simon Msuva.
Ngoya
walifanya shambulio la nguvu katika dakika ya tisa na nusura wafunge bao,
lakini Rakotoariamanana Falinirino alishindwa kufunga licha ya kuwa yeye na
kipa na kupiga nje.
Kikosi Yanga
Deogratius
Munish, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondan, Vecent Bossou, Justine Zullu,
Simon Msuva, Thaban Kamusoko, Deus Kaseke, Obrey Chirwa na Emmanuel Marrine.
No comments:
Post a Comment