SIMBA imeiengua
Yanga kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga
Tanzania Prisons kwa mabao 3-0 na kufikisha pointi 51.
Kwa ushindi
huo, Simba wameiacha Yanga na pointi zake 49 baada ya mabingwa hao watetezi jana
kutoshuka dimbani baada ya kuwa na mechi ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya
timu ya Comoro.
Simba huenda
ikakalia kiti hicho kwa muda kama Yanga watashinda mchezo wao dhidi ya watani
zao hao wa jadi katika mchezo utakaofanyika Februari 25 kwenye Uwanja wa Taifa.
Yanga
inarudiana na Wacomoro Jumamosi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika
mchezo huo wa jana, Simba waliandika bao la kwanza katika dakika ya 18
lililofungwa na Juma Luizio baada ya kupigwa kona ya `nje’ kabla ya mpira kumkuta mfungaji aliyeujanza wavuni.
Dakika 10
baadae Simba waliandika bao la pili kupitia kwa Ibrahim Ajibu akiunganisha
wavuni krosi ya Laudit Mafugo.
Wekundu hao
wa Msimbazi waliandika bao la tatu lililofungwa na Laudit Mavugo kwa kichwa
akiunganisha krosi ya Ajibu.
Simba: Daniel Agyei,Method Mwanjale/Mwinyi
Kazimoto, Javier Bukungu, Mohamef Hussein, Novalty Lufunga, Said Ndemla, James
Kotei, Mzamiru Yassin, Ibrahim Ajibu/Pastor Athanas, Laudit Mavugo na Juma
Luizio/Shiza Kichuya.
Prisons: Laurian Mpalile, Aron kalambo, Salum
Kimenya, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elifadhili, Lambart Sabiyanka,
Kazungu Nchinjayi/Kassim Hamis, Victor Hangaya, Mohamed Samata na Benjamin
Asukile/Meshaki Selemani.
No comments:
Post a Comment