Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) hatua ya 6 Bora ambayo ilikuwa ianze Febrauri 18, 2017
Uwanja wa Karume, imesogezwa mbele kwa muda wa juma moja.
Ligi hiyo sasa itaanza rasmi Februari
26, 2017 kwenye uwanja huohuo wa kumbukumbu ya Karume, Ilala mahali zilipo
ofisi za TFF. Hii ni kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wetu.
Timu sita zilizofanikiwa kufika hatua
ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair
Play ya Tanga kutoka Kundi “A” wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya
Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kutakuwa na
mechi mbili kila siku katika kituo kimoja kwa mujibu wa kanuni. Kituo hicho ni
Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es Salaam ambako mchezo wa kwanza
utaanza saa 8.00 mchana wakati mwingine utaanza saa 10.00 jioni.
Ratiba mpya inaonesha kwamba siku ya
Februari 26, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na Mlandizi saa
8.00 mchana wakati saa 10.00 kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na Sisterz.
Ratiba kamili kwa mechi inazofuata itatolewa
wiki ijayo. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaomba radhi kwa
usumbufu wowote uliojitokeza au unaoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko
hayo.
No comments:
Post a Comment