Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, January 16, 2017

WANDISHI WAMUOGA AMINA DAR ES SALAAM, KUZIKWA TANGA KESHO









WATU mbalimbali leo walikusanyika nyumbani kwa marehemu Amina Athuman Ukonga Banana, Dar es Salaam kutoa heshima za mwisho kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda kuzikwa Tanga kesho.
Akizungumza kwa niaba ya wandishi wa habari za michezo, Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa habari, Juma Pinto alisema tasnia imeondokewa na mwandishi mchapakazi na mwadilifu.
“Kwa niaba ya wandishi wa habari za michezo tumepokea kwa masikitiko msiba wa Amina kwani alikuwa mchapakazi na alipenda kushirikiana na wenzake,” alisema Pinto.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Uhuru Publications, Angela Akilimali alisema wamepoteza mfanyakazi hodari na pengo lake halitazibika.
“Amina alipatwa na umauti wakati akitimiza wajibu wake visiwani Zanzibar hiyo inadhihirisha wazi alikuwa mfanyakazi anayependa kutimiza wajibu wake bila kujali hali yake,” alisema Angela.
Amina alikuwa visiwani Zanzibar kikazi, kuripoti michuano ya Kombe la Mapinduzi na Mwenyezi Mungu akamuongoza kuifanya kazi yake vizuri mwanzo hadi mwisho.

Amina alipatwa na umauti usiku wa kuamkia Jumapili  akiwa amelazwa khospita na alijifungua mtoto wa kiume ambaye kwa bahati mbaya alikwishafariki dunia.

Amina ameacha motto mmoja wa kike. Mungu ampumzishe kwa amani Amina Athumani. 


No comments:

Post a Comment