Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 17, 2017

LUIZIO AKIRI UKUTA WA MTIBWA SUGAR KUWA MGUMU LAKINI ATATOA HIVYO HIVYO



KESHO kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro kutakuwa na mechi ya Simba na Mtibwa Sugar lakini mshambuliaji Juma Liuzio amekiangalia kikosi chake cha zamani kutoka Manungu na kutamka kuwa beki yao ni ngumu ila watatoboa tu.

Liuzio ambaye amesajiliwa Simba kwa mkopo akitokea Zesco United ya Zambia itakuwa ni mechi yake ya kwanza kukutana na Mtibwa Sugar tangu alipoachana na timu hiyo miaka miwili iliyopita akitimkia Zambia ingawa tayari amecheza mechi moja ya ligi kuu.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 44 wakati Mtibwa Sugar wao wana pointi 30 zilizofanya washike nafasi ya tano kwenye msikamo wa ligi hiyo huku ikitaka kuendeleza umwamba kwenye uwanja wa nyumbani ambao mara kadhaa umekuwa ukiisumbua Simba.

Akizungumza mshambuliaji huyo alisema kuwa Mtibwa Sugar sio timu ya kuibeza ipo vizuri na wapo nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hivyo hawatakubali kupoteza mechi hiyo na kwamba hata wao watapambana kuhakikisha ushindi unapatikana na kuendelea kukaa kileleni.

"Mechi itakuwa ngumu sababu Mtibwa ni timu nzuri na ukizingatia wapo nafasi nzuri pia nadhani haina mabadiliko makubwa sana wachezaji wengi niliowaacha bado wapo pale. Safu yao ya ulinzi inayoongozwa na Salim Mbonde beki anayejiamini ipo imara.

"Ukiangalia kikosi cha kwanza cha Mtibwa kina sura mpya hivyo sio wote waliokuwa pamoja wanacheza kikosi cha kwanza na sidhani kama italeta shida sisi kupata ushindi," alisema Liuzio.

Wakati Liuzio ikiwa mechi yake ya kwanza kukutana na timu yake ya nyumbani, Mtibwa nayo msimu huu itaingia uwanjani bila kocha mkuu Salum Mayanga ambaye ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda wa Taifa Stars, hivyo kikosi hicho kitaongozwa na wasaidizi wa benchi la ufundi chini ya Zubery Katwila.

Kocha wa makipa, Patrick Mwangata amesema kuwa; "Hakuna tatizo lolote na wachezaji wanatambua umuhimu wa hiyo mechi sidhani kama Simba watapata ushindi kirahisi, tutacheza kwa utulivu na tunajua wapi tutaikamatia Simba,".

No comments:

Post a Comment