Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 24, 2017

SAKATA LA KESSY NA LUDOVIC WA MWADUI KUSIKILIZWA WIKI IJAYOBEKI wa Kagera Sugar, Godfrey Taita anapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa kosa la kuwavamia waamuzi baada ya mechi na kuwatolea lugha chafu na vitisho kwenye mchezo dhidi ya Mwadui FC uliochezwa kwenye Uwanja wa Shinyanga.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema Taita alifanya kosa hilo baada ya mchezo kumalizika lakini baadae alidhibitiwa na benchi la ufundi la timu yake na askari polisi kuingilia kati kumdhibiti.
"Kamati ya nidhamu itasikiliza shauri la Taita na pia kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF itasikiliza malalamiko ya Mwadui FC, Polisi Morogoro na Simba kuhusu Hassan Kessy," alisema Lucas
Polisi Morogoro inalalamika uhalali wa usajili wa mchezaji wa Stand United, Kheri Mohamed Khalifa na wachezaji wawili wa Njombe Mji kucheza mechi bila leseni na sakata la Simba kuhusu Hassan Kessy.
Pia maombi ya klabu ya Singida United kuhusu kubadilishiwa mwamuzi kwenye mechi yao yamepelekwa Kamati ya Waamuzi, wakati maombi ya Alliance Schools, Friends Rangers FC, The Mighty Elephant na Kariakoo FC yanayohusu uendeshaji yanashughulikiwa na Sekretarieti ya TPLB.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF inatarajiwa kukaa wiki ijayo kusikiliza malalamiko dhidi ya usajili wa wachezaji mbalimbali akiwemo mchezaji Venance Joseph Ludovic na Hassan Kessy wa Yanga.