Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 6, 2017

ORODHA ZA WASHINDI WA TUZO ZA CAF 2017


screen-shot-2017-01-06-at-9-43-00-am
Jana usiku kulikuwa na ugawaji wa tuzo za chama cha soka Afrika CAF zilizofanyika mjini Abuja nchini Nigeria tuzo hizi kwa mwaka huu zikimshuhudia nyota wa Leicester City Ryad Mahrez akiibuka kidedea tuzo ya mchezaji bora Afrika,huku msanii toka Tanzania Naseeb Abdul almaarufu Diamond Platnumz akituwakilisha kwa shoo kali,Shaffih Dauda inakuletea orodha kamili ya washindi wa tuzo na sababu za ushindi.
1.MCHEZAJI BORA AFRIKA:-Ryad Mahrez hakuna ubishi kuhusu Mahrez,kiwango chake msimu uliopita kilikua cha hali ya juu akiisaidua klabu yake kupata ubingwa wa Uingereza akipata kura 361 mbele ya Pierre Aubemeyang mwenye kura 313 na Sadio Mane aliyepata kura 186,msimu wa mwaka 2015/2016 aliifungia Leicester magoli 17.
2.MCHEZAJI BORA AFRIKA KWA LIGI ZA AFRIKA:-Dennis Onyango golikipa wa Mamelodi Sundowns akiisaidia kupata ubingwa wa vilabu Afrika,anachukua tuzo hii siku chache baada ya kipewa tuzo ya mchezaji bora nchini kwao Uganda,tuzo hii pia imeshawahi chukuliwa na Mtanzania Mbwana Alli Samata.
3.KOCHA BORA:-Pitso Mosimame kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Bafana Bafana ,msimu uliopita ulikuwa mzuri kwake akishuudiwa akiipa ubingwa wa vilabu timu yake ya Mamelodi Sundowns.
4.MCHEZAJI BORA CHIPUKIZi:-Kati ya tuzo zilizokuwa ngumu hasa ukizingatia ubora wa chipukizi wengi Afrika walivyosumbua Ulaya lakini Alex Iwobi amepata tuzo hii kutolana na kiwango chake akiwa na Arsenal lakini pia na timu ya taifa Nigeria.
5:-TIMU BORA YA TAIFA:-Ilikuwa ni “suprise” kwa watu wengi pale Uganda ilipopewa tuzo hii lakini siku za karibuni wamekuwa katika kiwango kizuri wakifuzu michuano ya AFCON lakini pia wameweza kutoa mchezaji bora kwa wachezaji wanaocheza ligi za Afrika bila shaka walistahili tuzo hii.
6.KIPAJI CHA MWAKA:-Kelechi Iheanacho mpira usingetenda haki kama bwanamdogo huyu angetoka kapa,Iheanacho amekua mchezaji muhimu Man City msimu huu na hata uliopita kwani amekuwa akifunga magoli muhimu mara nyingi anapopewa nafasi na kocha Pep Guardiola amekuwa akipenda kumtumia mara kwa mara.
7.KLABU BORA YA MWAKA:-Mamelodi Sundowns hakuna hata chembe ya shaka kuhusu hili kwani hakuna asiejua walichokifanya msimu uliopita,ni klabu bora iliyojijenga ndani na nje ya uwanja wakiwa na kocha bora Mosimane na wachezaji bora waliwafunga Zamalek na kufanikiwa kubeba kombe la vilabu Afrika.
8.REFA BORA:-Bakary Gassama alichezesha fainail ya klabu bingwa Afrika kati ya Zamalek na Mamelodi Sundowns raia huyu wa Gambia mwenye miaka 37 ulikuwa msimu bora kabisa kwake 2015/2016 japo alianza kazi ya ukocha mwaka 2007.
9.TIMU BORA YA WANAWAKE:-Chini ya kocha wao Florence Omagbemi timu hii ijulikanayo kama Super Falcons waliweza kushinda mashindano ya Afrika kwwa wanawake.
10.MCHEZAJI BORA WA KIKE:-Asisat Oshoala aliisaidia Super Falcons kubeba ubingwa wa Afrika alizaliwa mwaka 1994 na magoli yake ndio yaliibeba sana timu yao ya taifa ya wanawake.Oshoala pia ni mchezaji wa timu ya wanawake ya Arsenal.
11.KIKOSI BORA CHA CAF:-1,Denis Onyango(Uganda),
2.Serge  Auirer(Ivory Coast)
3.Salif Coulibaly(Mali)
4.Eric Baily(Ivory Coast)
5.Joyce Lomalisa(Conho Brazaville)
6.Khama Billat(Zimbabwe)
7.Mohamed Salah(Misri)
8.Ryad Mahrez(Algeria)
9.Islam Slimani(Algeria)
10.Sadio Mane(Senegal)
11.Alex Iwobi (Nigeria)