Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 6, 2017

ISSA HAYATOU KWENYE KASHFA YA RUSHWA KAMA BLATTER



Mamlaka zinazosimamia mashindano mbalimbali nchini Misri zimethibitisha kuwa Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF,  Issa Hayatou atafikishwa kwa mkurugenzi  wa mashitaka kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili huku zikiwemo zile za utoaji haki za matangazo ya ligi mbalimbali.
Mamlaka hizo zimebainisha kuwa Hayatou alikiuka kipengele namba vifungu (A), (B), (C), (D), (E) za sheria za uhifadhi na ulinzi wa mashindano, baada ya kukiuka matakwa ya kazi yake na kuwapa haki za matangazo kampuni ya Lagardere Sports pekee pasipo kuweka wazi ili kampuni nyingine zenye uwezo pia zijitokeze.
Ripoti inasema kuwa Hayatou aliwapa Lagardere haki za matangazo kwa miaka 12 kuanzia mwaka 2017 mpaka mwaka 2028. CAF ilisaini kandarasi na Lagardere mwezi June 2015, ikiwa ni takribani mwaka mmoja kabla makubaliano ya haki hizo hayajakwisha. Ni sahihi pia kusema kuwa CAF iliwapa haki hizo Lagardere mwaka  2008 mpaka 2016, ikimaanisha kampuni hiyo imepewa mzigo huo kwa miaka 20.
Haki hizi hazikuwa kwa upande wa urushwaji matangazo kwa njia ya satellite peke yake bali hata kwa wenye matumizi ya tovuti, na sio kwa Misri na Afrika peke yake, bali dunia kwa ujumla.
Mamlaka hizo za mashindano ya Misri, zimeomba  CAF kuchukua hatua za haraka kutokana na kifungu cha sheria namba 20 kilichopo kwenye sheria za mashindano, ikiwemo kuvunja mkataba uliopo kati yake na Lagardere kutokana na matokeo iliyonayo kwa Misri.
Mamlaka hiyo pia imetoa ruksa kwa kampuni ya BeIn media pamoja na kampuni nyingine zilizoomba haki ya kurusha matangazo mubashara kuendelea kufanya hivyo hasa kwa ajili ya mashindano ya mataifa ya Afrika, 2017 AFCON itakayoanza January 14.
CAF iabadili pia namna haki za matangazo za mashindano mbalimbali zinavyouzwa nchini Misri katika mantiki ya kugawanya vifurushi vinavyohakikisha kutengeneza mazingira yatakayovutia mahsindano hayo kurushwa na vituo.
Mamlaka za mashindano zinaweka wazi kuwa CAF ina mlengo wa kuhakikisha inalinda na kusimamia sheria za mashindano na pia inatakiwa  kufuata hivyo kulingana na makubaliano yaliyopo kati ya serikali ya Misri na CAF.
Na kwa taarifa zinazoendelea kutoka ni kuwa CAF ina mpango wa kuhamisha makazi yake kutoka nchini Misri, lakini mamlaka ya mashindano imesema kuweza kufanya hivyo asilimia 75 ya wanachama ambao ni nchi 54 wanatakiwa kupiga kura kukubali kwenye mkutano mkuu kutokana na sheria za CAF kifungu namba 1.

No comments:

Post a Comment