Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, December 21, 2016

YANGA ILIKUWA JASHO NA DAMU UHURU








YANGA leo wamefanya mazoezi ya jasho na damu kwa muda wa saa moja kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
Katika mazoezi hayo ambayo kitaalumu yanaitwa saketi wachezaji walionekana kuchoka lakini walifanya hadi mwisho na kuhitimisha na kucheza mpira kwa dakika 30
Saketi ni muunganiko wa mazoezi mengi kwa pamoja sehemu nyingine yanahusisha mpira na sehemu nyingine bila mpira kwa mazoezi hayo mchezaji anapata stamina, unyumbufu na uvumilivu vitu ambavyo ni muhimu kwenye mechi.
Akizungumza baada ya mazoezi, kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi alisema ni maandalizi ya mchezo dhidi ya African Lyon utakaochezwa kesho kwenye uwanja huo.
“Maandalizi ni mazuri na wachezaji wana ari na kwenye mazoezi umeona wamefanya vizuri japo yalikuwa na ugumu lakini kwa ujumla tupo vizuri,” alisema Mwambusi
Pia Mwambusi alisema kipa Beno Kakolanya ndie pekee aliye majeruhi kwani anasumbuliwa na nyonga
Naye nahodha msaidizi, Haruna Niyonzima alikiri kwenye ligi hakuna timu ndogo hivyo wanachukulia uzito mchezo huo na kisaikolojia wapo vizuri kwa sababu wamelipwa stahili zao.
“Unapoona wachezaji wanafanya mazoezi ina maana wamelipwa haki zao hivyo kazi yetu ni kuhakikisha mchezo na African Lyon tunashinda ili tuwape mashabiki wetu zawadi ya krismasi,” alisema Niyonzima
Habari za ndani zinasema wachezaji hao wamelipwa posho za mchezo wao na JKT Ruvu huku wakiahidiwa kulipwa mshahara muda wowote kabla ya Ijumaa.
Yanga ambayo ina pointi 36 kwenye nafasi ya pili inacheza na African Lyon inayoshika nafasi ya 12 ikiwa na ikiwa na pointi 18 baada ya kucheza michezo 16 kila moja.

No comments:

Post a Comment