Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 20, 2016

KAMBI YA TIMU YA TAIFA YA U-14 YAVUNJWA LEO




KAMBI ya Timu ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 14 inayojiandaa na fainali za Vijana za Afrika 2019, imevunjwa leo kwa ajili sikukuu za krismasi na mwaka mpya
Akizungumza na gazeti hili, kocha wa timu hiyo, Oscar Mirambo alisema kuwa wamekaa kambini kwa siku 14 na kufanikiwa kucheza michezo minne ya kirafiki na kushinda yote.
“Wachezaji wameruhusiwa kwenda nyumbani kuungana na wazazi wao kwa ajili ya kusheherekea sikukuu na watarejea Januari mwakani,” alisema Mirambo
Pia Mirambo alisema kambi yao ilikuwa na mafanikio na hiyo ni dalili njema kuelekea kuwa mwenyeji wa fainali za vijana za Afrika zitakazo fanyika 2019 hapa nchini.
Kambi hiyo ilianza Desemba 4 ikiwa na wachezaji 22 lakini kocha Mirambo anasema wanatarajia kuongeza wachezaji wengine hadi wafike 35 ndio maana wanafanya ziara mikoani.
Wakati timu hiyo ikiwa kambini ilifanya ziara Morogoro ambapo walicheza na Moro Kids na kushinda mabao 3-1 na Zanzibar walicheza na Kombaini ya Vijana wa Unguja Kaskazini mabao 8-1, Kombaini ya Kusini waliifunga mabao 16-0 na Jumapili waliifunga Burundi mabao 3-1.
Naye Mwenyekiti wa Soka la Vijana, Ayoub Nyenzi alisema Tanzania itakuwa mwenyeji wa fainali mwaka 2019 hivyo wapo katika mchakato wa kutafuta timu na uteuzi utakoma mwishoni mwa mwaka 2017 kwani wanatarajia kupata timu ya uhakika itakayotoa ushindani.
“Mwaka 2019 kutakuwa na fainali za Afrika vijana, na sisi Tanzania ndio wenyeji kwasababu tuliomba CAF tukakubaliwa, ni lazima tutakuwemo kwa vile ni wenyeji, kwahiyo tumeona bora tuanze maadalizi mapema na ndio maana tumeanza tangu mwaka 2014 ili tupate timu imara katika mashindano hayo,”. alisema Ayoub.

No comments:

Post a Comment