Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 20, 2016

WACHEZAJI YANGA WANOGESHA MGOMO SIKU YA PILI SASAWACHEZAJI wa Yanga wameendelea na mgomo wao kwa siku ya pili wakishinikiza walipwe mshahara wa Novemba.
Leo ni wachezaji wawili tu walioonekana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambao ni kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ na beki Oscar Joshua.
Pia makocha George Lwandamina na wasaidizi wake, Noel Mwandila Mzambia na  Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali, Meneja Hafidh Saleh, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli Jacob Onyango na Mtunza Vifaa Mohammed Omar ‘Mpogolo’.
Akizungumzia sakata hilo Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema wachezaji wanataka kulipwa mshahara mwanzoni mwa mwezi badal ya mwisho wa mwezi.
Kinacholeta tatizo hapa ni kubadilika kwa mfumo wa ulipaji, badala ya mwisho wa mwezi, sasa tunalipa mwanzoni mwa mwezi. Sasa wachezaji wanataka mishahara ya Desemba walipwe mapema kwa sababu ya sikukuu,”alisema Baraka
Mgomo huo ulianza ghafla jana baada ya wachezaji kufika Uwanja wa Uhuru jioni, lakini wakagoma kuingia uwanjani kufanya mazoezi.
Uongozi wa Yanga umekanusha kuwapo kwa madai ya mishahara ya Novemba na kwamba wachezaji wanagoma wakitaka walipwe mapema mishahara ya mwezi huu, Desemba.

Taarifa zaidi zinasema kutakuwepo na kikao mchana kati ya wachezaji na viongozi wa Yanga kulitafutia ufumbuzi suala ili usiathiri maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya African Lyon utakaochezwa Ijumaa katika Uwanja wa Uhuru.