Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 27, 2016

HATIMAYE FARID MUSA NAONDOKA KESHO





KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Farid Mussa anatarajia kuondoka nchini kesho usiku kuelekea Hispania baada ya kutumiwa tiketi ya ndege na klabu ya Tenerife inayoshiriki ligi daraja la pili
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffa Idd alisema Farid ataondoka saa 5 usiku kwa ndege ya KLM ambapo atapitia Amsterdam, Barcelona hadi kufika Tenerife na kujiunga na timu hiyo kwa mkopo.
"Kesho  saa 5 usiku Farid ataondoka kwenda Hispania kwa ndege ya KLM kujiunga na timu ya Tenerife inayoshiriki ligi daraja la pili, tayari ametumiwa tiketi kwa ajili ya safari hiyo na sisi Azam tunamtakia kila la kheri katika maisha mapya ya soka" alisema Jaffa huku akiwaonesha wandishi tiketi hiyo.
Farid anakwenda Tenerife kwa mkopo hivyo Azam FC watakuwa wanamlipa stahiki zote ikiwemo  mshahara kwa mujibu wa mkataba walioingia na klabu hiyo.
Awali Tenerife walitaka kumsajili winga huyo kwa mkataba wa moja kwa moja baada ya kufaulu majaribio lakini dau ambalo walitaka kutoa lilikataliwa na Azam kwakuwa lilikuwa dogo na baadae walikubaliana kumchukua kwa mkopo.
Kuondoka kwa Farid kunaweza kufungua milango kwa wachezaji wengine wa Tanzania kwavile atautangaza vyema mpira wa nchi hii.

No comments:

Post a Comment