Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 27, 2016

BEKI WA SIMBA APIGA HAT TRICKMENEJA wa Simba, Musa Mgosi amemtumia salamu za pongezi, beki wao wa kimataifa Juuko Murshid baada ya mke wake kujifungua watoto mapacha watatu juzi.
Akizungumza na gazeti hili, Mgosi alisema ni jambo la heri na kumshukuru Mungu kwa kumjaalia mwezetu kupata watoto mapacha na wanamwomba Mungu awape afya tele.
“Juuko yupo kwenye timu ya Taifa ya Uganda lakini tumepokea taarifa hizo njema kwa furaha hivyo tunampongeza sana,” alisema Mgosi
Kwa mujibu wa Mgosi mke wa Juuko anaitwa Ruth na anaendelea vema yeye pamoja na watoto.
Juuko hajajiunga na Simba katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara kwa sababu yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ kujiandaa na mashindano ya Afrika yatakayofanyika Gabon.