Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 27, 2016

ZAHORO RUKSA KUKIPIGA MBEYA CITY BAADA YA KUPATA ITC



MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Zahoro Pazzi anatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza akiwa na timu hiyo Desemba 31, dhidi ya Mbao FC, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Zahoro ambaye alisajiliwa na timu hiyo kwenye dirisha dogo amesema anamshukuru Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Jamal Malinzi kwani amepata ITC yake iliyokuwa ikishikiliwa na FC Lupopo ya DR Congo kwa miaka miwili sasa.
“Namshukuru Rais Malinzi kwa kusikia kilio changu kwani niliandika kwenye mtandao wa kijamii kuhusu ITC yangu iliyokuwa inashikiliwa na FC Lupopo kinyume na utaratibu na alipoisoma alinitafuta akaniahidi ndani ya siku saba nitaipata, nashukuru nimeipata,” alisema Zahoro.
Pia Zahoro amewataka wachezaji wenzake endapo wana tatizo wasiogope kulifikisha ngazi za juu kwani watapata msaada kwa wakati.

“Mimi ningeogopa naamini hadi leo nisingekuwa nimepata ITC yangu lakini baada ya kumwomba Rais Malinzi msaada alikutana na mimi nikamweleza sakata lote na kuahidi kulishughulikia ndani ya siku saba na kweli nimepata,” alisema Zahoro.


Zahoro hajawahi kucheza FC Lupopo lakini ITC yake ilitolewa kwa uongozi wa timu hiyo na mmoja wa viongozi ndani ya shirikisho jambo ambalo Zahoro anasema ilikuwa kinyume kwani hawakufikia makubaliano ya kwenda kucheza huko.

No comments:

Post a Comment