Saturday, September 3, 2016
YANGA YAAMRIWA NA FIFA KUJIUNGA NA GPX KABLA YA JUMATATU
YANGA ni miongoni mwa timu tisa za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo zimeagizwa na Shirikisho la Soka Duniani 'FIFA' kujiunga mara moja na mfumo unaoitwa GPX yaani Global Players Exchange ambao malengo yake ni kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji kabla ya jumatatu.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Alfred Lucas, alisema kwa mara nyingine FIFA imeagiza na imeleta orodha ya klabu tisa za Ligi Kuu na Klabu sita za Ligi Daraja la Kwanza kujiunga mara moja na mfumo huo unaoitwa GPX.
"Majina ya klabu za ligi kuu ni African Lyon na Yanga za Dar es Salaam, Mtibwa Sugar ya Morogoro, Ruvu Shooting na JKT Ruvu za Pwani, Mbeya City ya Mbeya, Ndanda ya Mtwara, Kagera Sugar ya Kagera na Mbao FC ya Mwanza", alisema Lucas.
Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza ni African Sports na Coastal Union za Tanga, Marsh Athletic ya Mwanza, Friends Rangers ya Dar es Salaam, JKT Oljoro ya Arusha na Polisi Morogoro ya Morogoro.
GPX ni kama mtandao wa kijamii unaoweza kulinganishwa na ‘WhatsApp’ unaofanya kuwa na mawasiliano ya karibu na FIFA imeagiza kuwa ni lazima mameneja wa TMS wa kila klabu na mashirikisho ya ya mpira wa miguu kujiunga na mtandao huo ambao unafanya kazi katika nchi husika pia unaunganisha ulimwengu wote.
Pia Lucas alisema mameneja wa usajili watakaokuwa tayari basi hawana budi kuwasiliana na Meneja usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kupata maelezo ya kina ya namna ya kujiunga na mtandao wa GPX.wa timu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili (SDL)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment