KAMATI
ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imeahirisha kikao chake kilichokuwa
kikae leo kutoa hukumu ya shauri la mchezaji Hassan Ramadhan Kessy.
Simba
inadai Kessy kavunja mkataba kwa kuanza kufanya mazoezi na Yanga sambamba na
kusajili katika timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam kabla ya mkataba
wake kufika mwisho Juni 15, 2016.
Akizungumza na wandishi wa habari
jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Alfred Lucas, alisema kwa
mujibu wa taarifa ya kamati hiyo, shauri hilo lilisikilizwa baadaye mwezi huu
katika tarehe itakayopangwa hapo baadaye kwa sababu akidi ya wajumbe wa kamati
hiyo haijatimia .
"Kamati imeahirisha kikao kwa
sababu akidi ni lazima wajumbe zaidi ya watatu wathibitishe kushiriki hivyo
hawajatimia ndio maana kikao hicho kimeahirishwa", alisema Lucas
Shauri hilo lilikuwa lisikiliwe
leo baada ya kushindikana kusikilizwa kwa shauri jingine linalohusu Klabu Simba
ikiilalamikia Klabu Yanga, kuingia mkataba na mchezaji Hassan Ramadhani Kessy wakati
bado ana mkataba na Simba.
Shauri la Simba dhidi ya Yanga lilishindika
kusikilizwa kwa sababu Yanga hawakutokea mbele ya kamati hiyo wakati wa
kusikiliza shauri hilo Agosti 24, kama
hawatatokea tena, shauri hilo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi
upande mmoja.
Kadhalika mashauri mengine
yatakayosikilizwa hapo baadaye ni pamoja na yale ambayo wahusika walipewa
nafasi ya kuyamaliza nje ya kamati lakini wakashindwa.
No comments:
Post a Comment