MEYA wa Manispaa wa Ilala, Charles Kayeko
ameipongeza Ashanti United kwa mafanikio waliyonayo na kuwapa msaada wa milioni
tano toka mfuko wa meya.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya mandalizi ya
timu hiyo toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Ashanti United, Almas Kasongo, meya
Kayeko alisema Manispaa ipo pamoja na wao na itakuwa inatenga bajeti ya michezo
kila mwaka.
"Michezo ndio iliyosaidia nchi hii kutafuta
uhuru na mimi Meya natamani tuwe na timu ya soka kama ile ya Kampala au Nairobi
ambazo zinatangaza majiji yao kimataifa na nyie mnafahamu Ilala ndio
Tanzania", alisema Kayeko.
Pia Kayeko alionesha wazi dhamira aliyonayo ya
manispaa hiyo kumiliki timu kama ilivyo Mbeya City kusema ameshaanza mchakato
wa kutafuta timu na kuahidi kulifikisha kwenye baraza la madiwani swala la
Ashanti na endapo watakubalia basi chaguo lao litakuwa Ashanti kwani ni timu ya
Ilala na chimbuko lake ni Ilala.
Awali akisoma taarifa Makamu Mwenyekiti wa Ashanti
United, Almas Kasongo alisema timu yao inakabiliwa na mandalizi ya ligi daraja
la kwanza inayotarajiwa kuanza Septemba 24 na kusema ili iweze kucheza ligi
inatakiwa kuwa na milioni 100.
"Mpaka sasa tuna milioni 24 na ili tucheze ligi
tunatakiwa kuwa na mil 100 hivyo pungufu ni milioni 76", alisema Kasongo
Pia Kasongo alisema bodi na kamati ya utendaji ya
timu hiyo imejitahidi kuomba msaada kwa watu mbalimbali na kilichopatikana ni
hizo milioni 24 hivyo wanahitaji msaada zaidi.
Ashanti United
ilishawahi kushiriki ligi kuu 2004-2007 na kushuka ligi daraja la kwanza 2008
hadi 2012 na ikapande tena ligi Kuu 2013-14 na kushuka hadi leo
No comments:
Post a Comment