Tuesday, August 9, 2016
YANGA YAPEWA SIKU MBILI KUWASILISHA UTETEZI WAKE ILI ISISHUSHWE DARAJA
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa siku mbili kwa klabu ya Yanga kueleza sababu za kushindwa kuwasilisha usajili pamoja na Coastal Union ya Tanga.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa alisema dirisha la usajili kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/2017 lilifungwa saa 6.00 usiku wa Jumamosi Agosti 6, 2016.
"Klabu ya Yanga na Coastal Union hazijawasilisha usajili wao lakini timu nyingine saba zina kasoro kwenye usajili hivyo TFF inasuburi barua za utetezi wa klabu ambazo hazikukamilisha zoezi la usajili ili iutume utetezi huo FIFA na endapo itaona unamashiko itatoa maamuzi yake", alisema Mwesigwa.
Mwesigwa alisema usajili unafanywa kwa njia ya mtandao, mfumo wa mtandao unaoitwa Transfer Matching System (TMS) ambao chombo chake cha kutunza kumbukumbu kipo Makao Makuu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) -Uswisi.
Kabla ya Usajili
Kabla ya kuanza kwa usajili Juni 15, 2016 Shirikisho liliandaa mafunzo ya usajili kwa klabu zote 64 ambapo kila klabu ilitakiwa kupeleka watendaji wawili kutoka ili kuongeza ufanisi na kuondoa kasoro ambazo zimekuwa zikijitokeza lakini Yanga na Simba hazikupeleka mtu kwenye mafunzo.
Klabu ambazo zilishindwa kufanya usajili huo kwenye mtandao ziliomba msaada TFF huku Mwesigwa akiitaja timu ya Mkamba Rangers kuwa ilituma mtu TFF kusaidiwa kufanya usajili.
Usajili wa mfumo pepe ni utaratibu wa FIFA na imesaidia kuondoa ujanjaujanja wa viongozi au watendaji kusema faili limeibiwa kumbe ni ujanja wa kumpeleka mchezaji kwenye timu nyingine.
Kusogeza dirisha
Katika kuomba dirisha kufunguliwa kuna gharama ambazo zinatakiwa kulipwa mfano katika uhamisho wa Emanuel Okwi pasi ya kusafiria ilichelewa kupakia na kufanya TFF kutozwa faini dola 5000 ambazo ni zaidi ya milioni 10 za kitanzania.
Mwesigwa amezitahadharisha timu endapo dirisha litafunguliwa zitakabiliwa na faini ya dolla 500 kwa kila mchezaji na faini nyingine inakwenda kwenye shirikisho na kusema pamoja na faini hiyo ni wajibu wao kuendelea kuwasiliana na FIFA ili kuomba dirisha kufungulia.
Klabu za Yanga, Cooastal Union, African Lyon, Kiluvya United, Mashujaa, Friends Rangers, Abajalo, Kitayosa na Mvuvumwa ambazo hazikuzituma usajili wake kuandaa utetezi utakaokwenda TFF ambao utatumwa FIFA yenye mamlaka ya kufungua dirisha, na utetezi huo ukikataliwa timu husika inabidi ishuke daraja ambalo halimo kwenye usajili wa mfumo wa TMS.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment