Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 13, 2016

YANGA YAFUFUA MATUMAINI BAADA YA KUIFUNGA MO BEJAIA 1-0 TAIFA


TIMU ya Yanga leo imeifunga  Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria bao 1-0 katika mchezo wa marudiano kundi A kombre la shirikisho barani Afrika uliochezwa  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao hilo la pekee la Yanga limefungwa na Amissi  Tambwe kwenye kipindi cha kwanza na kuifanya Yanga kupata ushindi wa kwanza baada ya mechi tano na kufikisha pointi nne.
Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake 10 baada ya mechi nne, ikishinda tatu na kutoa sare moja, ikifuatiwa na Bejaia na Medeama, ambazo kila moja ina pointi tano za sare tatu na ushindi mmoja. 
Kocha Mholanzi, Hans Pluijm alifanya mabadiliko ndani ya robo ya kwanza ya mchezo, baada ya beki wake, Andrew Vincent ‘Dante’ kuumia na kumuingiza mkongwe, Kevin Yondan.
Pia alimpumzisha beki wake wa kulia, Juma Abdul baada ya kipindi cha kwanza kufuatia kuumia nyama na kumuingiza kiungo Said Juma ‘Makapu’ aliyekwenda kucheza kama kiungo ea ulinzi, huku Mbuyu Twite akihamia beki ya kulia.  
Yanga itahitimisha mechi zake za Kundi A Kombe la Shirikisho kwa kumenyana na wenyeji TP Mazembe ya DRC mjini Lubumbashi Agosti 23, mwaka huu. 
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Said Juma ‘Makapu’ dk46, Mwinyi Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’/Kevin Yondan dk17, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na Deus Kaseke/Juma Mahadhi.
MO Bejaia; Chamseddine Rahmani, Ismail Benettayeb, Faouzi Rahal, Sofiane Khadir, Soumaila Sidibe, Zakaria Bencherifa, Mohamed Yacine Athmani, Morgan Betorangal, Sofiane Baouali, Amar Benmelouka na Kamel Yesli.